Mwanariadha wa Mbio ndefu kutoka Tanzania Gabriel Geay amesema anasubiria taarifa ya daktari wake kuhusu afya yake kama ataweza kushindana katika michuano ya Olimpiki msimu huu kutokana na kuwa majeruhi.
Geaya amesema kuwa kwa sasa anafanya mazoezi kulingana na maelekezo ya daktari na anatumaini kuwa atakuwa vyema mpaka siku ya michuano hiyo inayofunguliwa Julai 26, 2024, Paris Ufaransa.
Majeraha aliyoyapata ni katika eneo la Kifundo cha Mguu, hii ni kulingana Daktari wa imu hiyo Elias Mkongo.
Jumla ya Wanariadha wanne wamefuzu kuiwakilisha nchi kuiwakilisha nchi kwenye Olimpiki msimu huu ambao ni Magdalena Shauri, Alphonce Simbu, Gabriel Geay na Jackline Sakilu ambao watakimbia Agosti 10 na 11.