Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amemsimamisha kazi, Meneja wa usambazaji Maji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) Eng Thomas Ngulika kwa kushinda kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Waziri Aweso ametangaza uamuazi huo Jumanne tarehe 23 Julai 2024 akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro.
“Hatutokuwa tayari kuona mtu kwa maksudi anatoa taarifa za uongo, wakati yeye ndiye anayehusika katika hilo jambo, eneo la Tungi, nane nane na maeneo mengine wiki tatu hawakupata maji, namuuliza Mtendaji anaongea uongo wewe unamwambia moja mbili tatu karekebishe, anarekebisha leo watu wanapata maji”
“Huyu mtu wetu ambaye anahusika na suala la Technical atatupisha, bodi ipo hapa mumsimamishe mara moja la pili acha mimi niende kwenye kikao ipo timu yangu hapa inanifanyia kazi nitawasaidia lakini lazima twende” amesema Waziri Aweso