Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira na Mbunge wa Jimbo la
Uzini Khamis Hamza Chilo amesema elimu kubwa inahitajika kwa Wananchi
kuacha matumizi ya Mkaa na Kuni kwa matumizi ya kupikia hali
itakayopelelekea utunzaji wa Mazingira.
Kauli
hiyo ameitoa huko Machui wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya
machui mara baada ya kukamilika utafiti uliofanywa taasisi isiyo ya
serekali ya up skills foundation kutoka Tanzania Bara unaohusisha
matumizi ya nishati ya kupikia na ufahamu wa wananchi juu ya dhana ya
uchumi wa buluuu.
Amesema
wananchi wengi hawana uelewa wa matumizi sahihi ya nishati ya kupikia
na dhana ya uchumi wa buluu kwa kuacha matumizi ya kuni na mkaa
ambayo hupelekea uchafuzi wa Mazingira na kusababisha maradhi kwa
wananchi.
Aidha ameeleza
matumizi ya nishati ya gesi kwa kupikia majumbani itasadia kwa kiwango
kikubwa utunzaji wa Mazingira kwa nchi kavu na bahari.
Nae
Mwakilishi wa Jimbo la hilo Haji Shaaban Waziri amesema kufanyika kwa
utafiti huo katika kijiji cha Machui itasaidia kwa Serekali kufahamu
matumizi ya nishati ya kupikia kwa wananchi wanaoishi vijijini pamoja
na dhana ya uchumi wa buluu.
Aidha
ameeleza Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serekali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuondosha matumizi ya kuni na mkaa na
badala yake wananchi watumie nishati ya gesi kwa matumizi ya kupikia .
Amesema
matumizi ya nishati ya gesi ya kupikia ni salama na huepusha maradhi
yanayosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa ikiwemo kifua kikuu na homa
ya mapafu.
Nae katibu wa
app skills foundation Tinnah Didas Masaburi amesema utafiti huo
wanaoufanya unalenga kujua ufahamu wa jamii kuhusu dhana ya uchumi wa
buluu na matumizi ya nishati ya kupikia.
Pia
utafiti huo utaonesha ni kwa namna gani jamii inatambua njia ya
utunzaji wa Mazingira na kutoa Elimu ya matumizi sahihi ya nishati
isiyo na madhara kwa binaadamu.
Nao
wananchi wa Shehia ya Machui wameushukuru uongozi wa Jimbo la Uzini
kwa kuiteua Shehia yao kuwa sehemu ya utafiti huo ambao umewasaidia
kufahamu njia sahihi ya utunzaji wa Mazingira na dhana nzima ya Uchumi
wa buluu.
Utafiti huo
umefanyika katika Shehia ua Machui kwa Mkoa wa Kusini Unguja, Shehia ya
Matemwe Kigomani, Shehia ya Mkokotoni kwa Mkoa wa Kaskazini Unguja na
Shehia ya Mndo kwa Mkoa wa Mjini Magharibi.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamo Muungano na Mazingira Khamis Hamza Chilo (wa
tatu kushoto)Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Haji Shaaban Waziri (wa
kwanza kulia ) Mdau wa maendeleo ya Jimbo la Uzini Lucia Mwaipopo (wa
pili kulia) na Katibu wa App skills Foundation Tinnah Didas Masaburi
wakisikiliza maelezo mafupi yanahusu Mazingira, utumiaji wa nishati
sahihi ya kupikia na ufahamu wa dhana ya uchumi wa buluu kwa Sister
Agnes Paulo (wa pili kushoto)wa parokia ya Kanisa la Katoliki na Chuo
cha Utalii cha Machui.
Ujumbe
wa App Skills foundation ukiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini
Haji Shaaban Waziri akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Matemwe na
Mwenyekiti wa Kiwanda Mungu ndie hakimu cha kuchakata takataka na kuwa
mbolea Sulubu Kidogo Amour huko Matemwe ujumbe huo ulifika hapo kwa
lengo la kufanya utafiti wa utunzaji wa Mazingira, matumizi sahihi ya
nishati ya kupikia na ufahamu wa wananchi juu ya dhana ya uchumi wa
buluu.