Nairobi. Rais wa Kenya, Wiliam Ruto ameteua Baraza jipya la mawaziri akimjumuisha aliyekuwa Gavana wa Mombasa, Hassan Joho aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Madini na John Mbadi akipewa Wizara ya Fedha.
Baraza hilo limetangazwa leo Julai 24, 2024 zikiwa zimepita siku tano tangu litangazwe lile la awali Ijumaa Julai 19, mwaka huu akiwarudisha sita waliokuwa mawaziri katika baraza alilovuja.
Uteuzi wa sasa unafikisha mawaziri 20 kutoka 10 wa awali.
Mabadiliko hayo yanafanyika kufuatia maandamano ya vijana wa nchi hiyo wapinga ugumu wa hali ya maisha, ongezeko la kodi na kutotimizwa kwa ahadi alizozitoa Ruto wakati wa kampeni.
2. Salim Mvurya – Viwanda na Uwekezaji
3. Rebecca Miano – Utalii
4. James Wandayi – Nishati
5. Kipchumba Murkomen – Vijana na Michezo
7. Alfred Mutua – Kazi na Hifadhi ya Jamii
8. Wycliffe Oparanya – Maendeleo ya Ushirika wa Biashara zinazochipukia, na za Kati.
9. Justin Muturi – Utumishi wa Umma na Ufanisi
10. Stella Soi Lang’at – Masuala ya Jinsia.
Endelea kufuatilia Mwananchi