NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Dkt. Charles Msonde amesema kuwa, upatikanaji wa madarasa janja (smart classrooms) utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuongeza ufanisi wa ujifunzaji na ufundishaji nchini pamoja na kupunguza changamoto ya upungufu wa walimu.
Dkt. Msonde amesema hayo leo katika ofisi za Taasisi ya Elimu Tanzania Jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi iliyowakutanisha viongozi kutoka Shanghai na Tanzania ambao pamoja na kujadiliana masuala mbalimbali ya uboreshaji wa elimu, walijionea utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar.
Amesema kuwa katika kipindi hiki cha utekelezaji wa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa matumizi ya teknolojia ya darasa janja hayaepukiki na yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuwafikia walimu wengi nchi nzima.
Sambamba na hilo, amewashukuru Wakurugenzi kutoka Shanghai, Taasisi ya Elimu Tanzania pamoja na Kampuni ya EduTech kwa kuunganisha jitihada kwa pamoja katika upatikanaji wa madarasa janja yatakayosaidia katika utoaji wa mafunzo katika maeneo mengi kwa wakati mmoja.
Aidha, Dkt. Msonde amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Elimu nchini, Serikali kupitia OR-TAMISEMI imeelekeza halmashauri zote nchini kuhakikisha zina darasa janja moja mpaka matatu kadiri ya mahitaji yao, na kusisitiza kila Mkoa unapaswa kuwa na darasa janja moja ili kuzilisha shule zilizo kwenye halmashauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba amesema kuwa, darasa janja litasaidia kupunguza idadi ya walimu wanaohitajika kufundisha katika somo moja, hivyo kusaidia kukabiliana na changamoto ya upungufu wa walimu nchini.
“Kama tulivyoshuhudia katika zoezi la leo, mwalimu mmoja anafundisha somo la hisabati akiwa katika kituo cha Taasisi ya Elimu Tanzania na madarasa mengine yameunganishwa kutoka Kibaha na shule ya Tumekuja ya Zanzibar.” Amesema Dkt. Komba.
Akifafanua zaidi, Dkt. Komba amesema kuwa, Taasisi ya Elimu Tanzania iliingia makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Shanghai Normal ya uboreshaji wa ujifunzaji na ufundishaji wa somo la Hisabati na masuala mengine ya Elimu. Makubaliano haya pamoja na mambo mengine, yamechangia katika kuifahamu kampuni ya EduTech iliyofadhili madarasa janja manne, moja likiwemo TET, Dodoma, Kibaha na Zanzibar.
Aidha, Dkt. Komba amesema kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha kila halmashauri inakuwa na darasa janja kulingana na mahitaji, jambo litalosaidia kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji na utekelezaji wenye ufanisi wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA).
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi kutoka Wizara ya Elimu Tanzania, OR TAMISEMI, Mkurugenzi wa Elimu China, Viongozi wa TET, Walimu kutoka chuo Kikuu cha Shanghai, TET, shule za Olimpio, Diamond, Zanaki na Tambaza.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Dkt. Charles Msonde akizungumza katika hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Dkt. Charles Msonde akizungumza katika hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Elimu China, Wang Hao akizungumza katika hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Elimu China, Wang Hao katika hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) pamoja na Walimu wa shule za Olimpio, Diamond, Zanaki na Tambaza wakiwa katika hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
Walimu kutoka Chuo Kikuu cha Shanghai wakiwa katika hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) anayeshughulikia elimu, Dkt. Charles Msonde akiwa na baadhi ya viongozi wa mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Walimu wa shule za Olimpio, Diamond, Zanaki na Tambaza wakati wa hafla fupi ya majaribio ya utendaji kazi wa madarasa janja yaliyounganishwa kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Dodoma, Pwani na Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 24,2024 Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)