GAMONDI ATOA SIRI YA KUSAJILI WACHEZAJI HAWA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alieleza ushindani wa namba umeongeza kitu kikubwa kwa wachezaji na kuwafanya wawe na hari ya kupambana, kwani hakuna anaejiamini atapata nafasi kutokana na ubora wa kila mmoja wapo.

 

“Ninafurahia ushindani wa namba unavyoendelea kwenye kikosi changu kwani umewafanya wachezaji kujituma na kutafuta nafasi na hizo ni sifa za mchezaji anayecheza kwa malengo ambao ndio wapo sasa kwenye kikosi changu,”

 

“Kikosi tulichosajili ni kwa malengo yetu ya msimu ujao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na ya ndani, hivyo haiwezekani kumpunguza hata mmoja, ijapokuwa nafahamu zinakuja ofa nyingi kwa wachezaji wetu nyota, lakini hatukuruhusu waondoke na badala yake tulipambana kuwabakiza ili kulinda hesabu za msimu ujao.”

Related Posts