Makocha Pamba Jiji wabebeshwa mzigo

WAKATI Pamba Jiji ikizindua wiki ya tamasha lake litakalofanyika Agosti 10, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mlezi wa timu hiyo, Said Mtanda alisema Kocha Goran Kopunovic na wasaidizi wake walipewa uhuru kwenye usajili na matokeo yakiwa mabaya wataulizwa.

Pamba Day itanogeshwa na burudani mbalimbali ikiwemo mchezo wa kirafiki na timu ambayo itatajwa baadaye, utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi, uzinduzi wa jezi, huku viingilio vikiwa ni Sh50,000, Sh20,000, Sh10,000 na Sh3,000 mzunguko na tayari tiketi 5,300 zimeshauzwa.

Akizungumza juzi kwenye uzinduzi wa tamasha hilo, Mtanda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alisema hawakufanya usajili wa kujuana kwani wachezaji 900 walipewa nafasi ya kuonyesha uwezo mazoezini na wachache kupitishwa na kocha huyo.

“Tulisema maamuzi ya kocha yaheshimiwe aliowataka ndiyo waliosajiliwa, sisi siyo watalaam ni viongozi kazi yetu tutafanya nje ya uwanja. Lakini kocha aliyepewa dhamana na benchi lake la ufundi wakifanya vizuri watapongezwa,† alisema Mtanda na kuongeza;

“Wakifanya vibaya lazima tuwahoji tuone kama tunafaa kuendelea nao, lakini ukimpangia watu atakwambia ulimletea wachezaji ambao hawawezi kumpa matokeo maana yake atakuwa na nafasi ya kutukimbia.â€

Mtanda aliwataka wadau wa timu hiyo kuungana na kuacha maneno ya pembeni na lawama kwa sababu mchezaji waliyemleta hakusajiliwa, huku akitishia atakayeleta nongwa na kuihujumu timu hiyo watapambana naye.

“Tusiwe na nongwa tushikamane tuifanye timu yetu iwe ya kudumu, lakini hatutakubaliana na mtu yeyote atakayeweka masilahi yake mbele kuivuruga timu kwa faida zake hatutaoneana aibu kama noma na iwe noma,† alisema Mtanda.

Related Posts