Rais wa Marekani Joe Biden, amesema aliamua kujiondoa kwenye kinyanganyiro cha kutafuta muhula wa pili wakati wa uchaguzi wa mwezi Novemba, ili kukiunganisha chama chake cha Democratic, na kutoa fursa kwa kizazi kipya kutafuta uongozi wa nchi hiyo.
Biden amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya wiki iliyopita kumpendekeza Makamu wake Kamala Harris kuwa mgombea wa chama cha Democratic.