SIMON PATRICK AIBUKA NA ISHU YA WACHEZAJI KUTOROKA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

“Hizi changamoto za wachezaji wenye mikataba kutoroka timu zao ni matokeo ya ushabiki na wachambuzi wetu. Kwa sasa, kuna wimbi la wachezaji kutoroka na wengine kuwa na mikataba na timu zaidi ya moja kwa madai kwamba hawana furaha na wanaenda kutafuta fursa bora zaidi.

 

“Ushauri wangu kwa BMT ili kuokoa soka letu ni kuweka kanuni inayolazimisha mchezaji yeyote mwenye mkataba akihama kutoka klabu moja kwenda nyingine lazima kuwe na Mkataba wa Uhamisho (Transfer Agreement) au Mkataba wa Kusitisha kwa Pamoja (Mutual Termination Agreement) uliothibitishwa na BMT na kulipiwa ushuru wa stampu (Stamp Duty).

 

“Mchezaji au timu yoyote ikikiuka, basi mchezaji huyo asipewe kibali cha kucheza nchini, period. Bila hatua hiyo, migogoro ya wachezaji wenye mikataba haitaisha kamwe na TFF itaendelea kulalamikiwa bure,” Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga SC, Simon Patrick.

Related Posts