ATAPELI MILIONI 6 KWA KUJIFANYA USALAMA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linamshikilia Marco Daud Zagamba (32) wa Mbweni Zanzibar kwa kosa la Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo amewatapeli Wananchi watano na kujipatia fedha Tsh. milioni 6 akijifanya ni Mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na kwamba atawasaidia Watu kuwapa ajira kwenye Idara hiyo huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa.

 

Mtuhumiwa huyo kwa wakati tofauti amewatapeli Wananchi kwa kujifanya yeye ni Mtumishi wa Umma na kwamba atawasaidia kuwapatia ajira za Vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 

Kwa kutumia mbinu hiyo mtuhumiwa alijipatia fedha Tsh. 4,600,000 kutoka kwa Wananchi wanne Wakazi wa Zanzibar na katika hatua nyingine July 22, 2024 huko Maisara Zanzibar, alimtapeli Mwananchi Tsh. 1,400,000 akidai yeye ni Mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na kwamba atamsaidia kumpatia ajira kwenye Idara hiyo huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa.

 

“Mtuhumiwa huyo amefanya matukio ya utapeli kwa muda mrefu akitumia mbinu ya kuwa karibu na ofisi za Serikali ili kuwaaminisha anaowatapeli kuwa ni Mtumishi wa Taasisi hizo na anapofanikisha utapeli huo hutoweka, nitoe wito kwa Wananchi katika kipindi hichi ambacho Mkuu wa Jeshi la Polisi Afande IGP. Camillus Wambura ametangaza usaili kwa Vijana walioomba ajira za Jeshi la Polisi, wachukue tahadhari dhidi ya Matapeli ambao wanatumia fursa hiyo ili kujipatia kipato kwa njia isiyo halali”

Related Posts