Harriet Ampayire (23) mkazi wa Wilaya ya Kyotera Mkoa wa Kati nchini Uganda anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa kumkata sehemu za siri.
Inadaiwa kuwa Harriet alimkata sehemu za siri mpenzi wake Reagan Karamagi, Jumapili Julai 21, 2024 kisha kutoroka.
Msemaji wa Polisi Kanda ya Kusini, Twaha Kasirye amethibitisha kukamatwa kwa Harriet na kueleza kuwa atakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya upelelezi kukamilika.
Polisi wamesema kuwa Mtuhumiwa huyo alitaka kukimbia kwa kuvuka mpaka wa Mutukula ili kuingia Tanzania lakini walifanikiwa kumkamata