Meli ya mizigo yazama kwenye ufuo wa Taiwan, mabaharia 9 watoweka

Meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Tanzania “imezama” kusini mwa Taiwan na wafanyakazi wake tisa, raia wa Burma, hawajulikani waliko, wamesema leo Alhamisi maafisa wa kikosi cha zima moto katika kisiwa kinachojitawala kilichopigwa na kimbunga Gaemi.

“Walitoweka na walikuwa wakielea baharini,” Hsiao Huan-chang amesema, akiongeza kuwa meli nyingine ya mizigo imeitwa kuja kusaidi katika shughuli ya uokoaji na kwamba waokoaji watatumwa “wakati hali ya hewa itaruhusu”.

Related Posts