Viatu vya rapa Travis Scott “Jumpman Jack” kuanza kuuzwa mwishoni mwa mwezi huu

Viatu vya Travis Scott “Jumpman Jack” Jordan hatimaye vimetajwa tarehe ya kutolewa, na ni hivi karibu kabisa.

Kulingana na Highsnobiety, bidhaa hiyo itatolewa Aprili 30 na itapatikana tu katika rangi nyeupe na kahawia mwanzonina baadae yatajumuisha chaguzi za ziada za rangi.

Viatu hivyo vilizinduliwa kwa mara ya kwanza katika tangazo mwezi Februari, ikiambatana na onyesho la kushtukiza ambalo liliisha ndani ya dakika chache.

Bidhaa hiyo ya viatu inayozungumziwa sasa inauzwa kwa zaidi ya $2k kwenye tovuti za mauzo.

Mwaka jana, mzaliwa huyo wa Houston aliboresha ubunifu wake aliposimamia usanifu upya wa viatu vya Nike vya Mac Attack kwa ushirikiano na gwiji wa tenisi John McEnroe.

Licha ya ushirikiano ulioonekana kuwa na msukosuko ambao wengi walikisia uliandaliwa kwa ajili ya utangazaji, kiatu hicho kilitolewa kwa watu wengi kikiwa na rangi nyeupe, rangi ya fedha na nyeusi na yenye matundu na ngozi.

Related Posts