ABIRIA ZAIDI YA 1000 WAANZA SAFARI YA TRENI YA SGR DAR ES SALAAM HADI DODOMA

Matukio mbalimbali ya picha za abiria wakiwasili katika Stesheni ya Treni ya Umeme ya Reli ya SGR jijini Dodoma wakati treni hiyo ilipoanza safari yake ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma leo Julai 25, 2024.

Na.Alex Sonna-DODOMA

SAFARI ya kwanza ya treni ya kisasa ya umeme (SGR) kutoka Dar es Saalam kwenda Dodoma imeanza rasmi leo Julai 25,2024 ambapo abiria zaidi ya 1,000 wamesafiri na Treni ya kwanza kufanya safari hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwa treni hiyo kwa mara ya kwanza alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maeelekezo ya serikali.

“Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo mwaka jana kuwa ifikapo mwezi Julai mwaka huu lazima usafiri wa treni ya umeme kutoka Dar es Saalam kuja Dodoma uwe umeshaanza rasmi.

“Leo tumetoka Dar majira ya 12 asubuhi na kufika Dodoma majira ya saa nne asubuhi na hii ni kutokana na kuwa kuna eneo tulisimama sana kwa ajili ya kupisha na treni iliyotoka ,huku lakini kadri siku zinavyokwenda tutaendelea kuboresha changamoto ambazo zimejitokeza leo kama ilivyokuwa wakati tulivyoanza safari za Dar Morogoro”alisema Kadogosa

Aidha, amesema kuwa  katika safari hiyo ya kwanza kuja Dodoma,zaidi ya watu 1,000 wamesafiri na treni hii hivyo mwitikio wa abiria kutumia usafiri huo umekuwa mkubwa sana hali ambayo inawapa kazi ya kufanya ili kukidhi mahitaji.

“Leo treni ya asubuhi tayari imejaa ya jioni na ya kesho pia imejaa hivyo tutaendelea kuangalia mwenendo utakavyokuwa ili kuongeza safari kama ilivyokuwa katika safari za Dar Morogoro”amesisitia Kadogosa

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri ardhini (LATRA) Habibu Suluo, amesema wanaipongeza serikali kwa kufanikisha safari ya kwanza ya treni ya kisasa kutoka Dar es Saalam kuja Dodoma.

“Maono ya Rais wetu yametimia leo tumepokea kwa mara ya kwanza treni ya umeme kutoka Dar es Saalam sasa nitumie fursa hii niwaombe watanzania tutunze miundombinu hii ambayo serikali imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kufanikisha mradi huu wa kimakakati”amesema

Naye Mmoja wa abiria wa treni hiyo Amina Hassan, amesema usafiri huo wa treni ya kisasa utakuwa mkombozi kwa makundi yote kutokana na kuokoa muda wa safari tofauti na ilivyokuwa kwa usafiri mwingine.

Related Posts