WAKILI MWABUKUSI ASHINDA KESI YAKE DHIDI YA TLS – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

 

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Julai 26.2024 imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa imefunguliwa na Wakili wa kujitegemea Boniface Mwabukusi dhidi ya TLS (Chama cha Mawakili Tanganyika) ambapo Wakili Mwabukusi alikuwa anapinga maamuzi ya kamati ya rufani kumuengua kugombea nafasi ya Rais wa chama hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

 

 

 

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Mahakama imeridhika na hoja zilizotolewa na upande wa Mwabukusi ambapo sasa rasmi imetengua maamuzi ya kamati ya rufani ya TLS, hivyo kwa sasa Wakili Mwabukusi amerejeshwa kugombea nafasi ya Rais wa TLS,

Related Posts