“Kampeni ya Ni Balaaa inalenga kuwazawadia wateja wetu kila wanaponunua kifurushi (bando) au kufanya miamala kupitia M-Pesa na pia kutoa nafasi kwa washindi wa zawadi kuu, kupendekeza Shule za Msingi katika Jamii zao na Vodacom Tanzania itafanya maboresho katika maktaba za shule hizo kama vile kuwapatia vitabu, makabati ya kuhifadhia vitabu na samani za kusomea”, alisema Grace Chambua, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kutoka Vodacom Tanzania wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Kariakoo-Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Kampeni hii yenye kaulimbiu ya ‘Kila Mtu ni Mshindi’ inaanza mwezi huu wa Julai mpaka Oktoba mwaka huu huku ikiwa na washindi wa kila siku wa shilingi 100,000/-, washindi wa wiki wa shilingi 500,000/- huku wale wa mwezi wakiondoka na shilingi milioni moja, na washindi watano wa zawadi kuu ambao kila mmoja ataondoka na kibunda cha shilingi milioni 20!
Akielezea namna ya kushinda kupitia M-Pesa, Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa M-Pesa kutoka kampuni hiyo, alisema, “kila muamala unaoufanya kupitia M-Pesa katika kipindi cha kampeni unaongeza nafasi yako ya kushinda. Iwe unatuma pesa kwa familia, unalipia bili au unatumia M-Pesa super App kwa miamala na malipo ya kila siku.”
Mbeteni aliongezea kuwa kampeni ya ‘Ni Balaaa” itakuwa shirikishi ili kuwezesha kila mteja popote pale alipo bila kujali umbali wala hali yake ya kiuchumi kuibuka na ushindi wa aina tofauti.
“M-Pesa inamrahishia kila mtu kufanya miamala, ikiwemo wafanyabiashara kama nyie mliotuzunguka hapa Kariakoo. Yaani popote pale ulipo kila unapotumia M-Pesa basi moja kwa moja unaingia kwenye droo na hivyo kujiongezea nafasi ya kuibuka mshindi. Sisi tunasema Pesa ni M-Pesa na msimu huu “Ni Balaaa”, anamalizia Mbeteni.
Kwa kumalizia Bi. Chambua aliongezea kuwa kampeni hii itawagusa pia wamiliki wa biashara ndogo na za kati ambapo kwa kujiunga na SME Combo Bundles kutoka Vodacom sio tu zitawarahisishia shughuli zao za kibiashara, lakini pia zinawapa nafasi ya kushinda zawadi muhimu kama vile zana za usimamizi wa hesabu (inventory management system) au kamera za CCTV kwa ulinzi zaidi wa maeneo yao ya biashara.
Ni Balaaa! George Lugata (kushoto), Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji, Athumani Mlinga, Mkurugenzi wa Kitengo cha TEHAMA, Grace Chambua, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara na Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa M-Pesa wote kutoka Vodacom Tanzania Plc wakizindua kampeni ya “Ni Balaaa” iliyofanyika tarehe 25 Julai 2024 Gerezani – Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo ya miezi minne inalenga kuwazawadia wateja wa kampuni hiyo zawadi za kila siku shilingi 100,000, wiki shilingi 500,000, mwezi shilingi milioni moja na hatimaye kuwapata washindi wakuu watano ambapo kila mmoja atapata shilingi 20 milioni.