Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) inayoongoza kwa utengenezaji wa vinywaji hapa nchini inayo furaha kutangaza Mkutano wake Mkuu wa Mwaka utakaofanyikia katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius nyerere (JNICC).
Mkutano huu utaangazia maendeleo ya kifedha ya (TBL), mikakati na nafasi yake katika soko.Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali ambao watajadili maendeleo ya TBL na changamoto zilizoikabili Kampuni kwa mwaka wa fedha uliopita.
Ajenda muhimu katika Mkutano huu itakuwa ni uidhinishaji wa gawio la shilingi 537 kwa kila hisa (za jumla ya shilingi 158,445 milioni) kwa mwaka uliomalizika Desemba 31, 2023, ongezeko la asilimia 85 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Hii inaonyesha dhamira ya TBL katika kurudisha faida thabiti kwa wanahisa wake.Mwenyekiti wa Bodi ya TBL, Bw. Leonard Mususa, alisema, “Tunajivunia kutangaza kuwa licha ya hali ngumu ya uendeshaji mwaka 2023, ikijumuisha mvutano wa kisiasa kijiografia duniani na ongezeko la ushuru wa ndani, Tanzania Breweries Public Limited Company (TBL PLC) ilionyesha ukuaji thabiti na kutoa thamani kubwa kwa wanahisa wetu.
Utekelezaji wetu madhubuti wa mipango ya kimkakati na imani ya soko katika orodha yetu ya chapa mbalimbali ilisababisha ongezeko kubwa la mapato, kutuwezesha kuidhinisha na kusambaza gawio la TZS 537 kwa kila hisa—ongezeko kubwa zaidi la asilimia 85 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Mafanikio haya yanasisitiza dhamira yetu ya kuunda thamani ya muda mrefu kwa wanahisa wetu na kuimarisha nafasi yetu kama moja ya wachangiaji wakuu wa ukuaji wa uchumi wa Taifa.
“Vilevile, mkutano huo ulihusisha uidhinishaji wa uteuzi wa Kampuni ya PricewaterhouseCoopers kama wakaguzi wa nje kwa mwaka wa kifedha ujao unaoishia Desemba 31, 2024, ikionyesha dhamira thabiti ya TBL PLC kwa utawala bora wa kifedha na uwazi.
Viashiria Muhimu vya Utendaji:Ukuaji wa Mapato na faida: Kampuni ilishuhudia mwaka mwingine wa muendelezo wa ukuaji wa faida, Mapato yaliongezeka kwa asilimia 12 na faida ya uendeshaji kwa asilimia 4.
Ukuaji wa mapato ulisukumwa na bia na pombe kali.Kampuni inaendelea kutekeleza mkakati wake wa kibiashara ulio thibitishwa na kuongeza uwekezaji katika mauzo na masoko nyuma ya orodha yake ya chapa za bia na zaidi ya bia ili kutoa ukuaji thabiti na kuunda thamani ya muda mrefu.
Ununuzi wa ndani na Ajira: TBL hununua zaidi ya asilimia 74 ya malighafi zake kutoka ndani ya nchi, ikisaidia moja kwa moja na kwa njia nyingine katika kutengeneza ajira zaidi ya milioni moja katika mnyororo wake wa ugavi.
Mafanikio haya yameimarisha hadhi ya TBL kama mwajiri namba moja na mtengeneza bidhaa mkuu wa Tanzania.
Mchango wa Kodi: TBL ililipa shilingi bilioni 586 kwa Serikali mwaka 2023, ikilinganishwa na bilioni 528 kwa mwaka uliopita, ikithibitisha nafasi yake kama mmoja wa walipa kodi wakubwa wa Taifa.
Mkutano Mkuu wa mwaka una ahidi kuwa tukio lenye kuongeza ufahamu, likidhihirisha mafanikio ya TBL na kuweka msingi wa ufananisi wa baadae.
Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Leonard Mususa akizungumza na wanahisa wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa 51 wa mwaka wa Kampuni hiyo ambao ulifanyika jana kwenye kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.Mkutano huo uliangazia utendaji wa kifedha wa TBL PLC, mikakati na nafasi yake katika soko. Kushoto ni Katibu wa Kampuni Bi. Esther Kuja na kulia ni Mjumbe wa Bodi Bw. Phocus J. I. Lasway.