SOGGY NA DATAZ WASHINDA KESI, KULIPWA MILIONI 700 NA HBO – MWANAHARAKATI MZALENDO

Hukumu ya kesi ya wanauziki Sogy Doggy na Dataz dhidi ya Home Box Office ya Marekani imesomwa leo katika Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam na Wasanii hao kushinda kesi.

Wasanii hao wakiwakilishwa na kampuni ya Markel Advocates walifungua kesi mahakamani mnamo mwaka 2021 wakidai HBO kuutumia wimbo wao wa “Sikutaki tena” kwenye filamu yao ya “Sometimes in April” iliyochezwa na staa Idris Elba bila ruhusa au makubaliano na wasanii hao.

Hatimaye, wasanii hao leo wamepewa ushindi kwa kazi yao kuibwa hivyo, HBO wametakiwa kuwalipa zaidi ya shilingi milioni 700 na bado wana nafasi ya kukata rufaa, Sikutaki tena ni wimbo ulioimbwa na Dataz akimshirikisha Soggy Doggy na ulitoka nwanzoni mwa Mwaka 2000 ukirekodiwa katika Studio za Soundcrafters chini ya mtayarishaji Enrico.

Credit : Simulizi na Sauti (Instagram)

#KonceptTvUpdates

Image
Image

Related Posts