HUKO kwenye Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) mambo ni moto na unaambiwa eti ukifunga mbele ya mchezaji Haji Mbegu wa Dar City au Haji Mbegu wa UDSM Outsiders basi wewe lazima utaonekana ni shujaa katika mchezo wa mechi husika kutokana na umahiri wao wa kukaba.
Mbegu anayecheza namba nne (power forward), akiwa mahiri kwa kukaba, kucheza ndani ya uwanja, kuchezesha wenzake na kufunga vilevile, huku kwa Brown, ana uwezo wa kuchukua mipira yote golini kwake ya (rebound) na kufunga kwa mpinzani.
Ubora wa wachezaji hao unaonekana, ni pale wanapowadhiti wachezaji wanaocheza nafasi ya mbele wa timu pinzani wasilete madhara katika goli lao .
Akimzungumzia Mbegu, kocha wa timu ya taifa, Mohamedi Mbwana alisema kuwa mchezaji huyo ana kila kitu cha uchezaji ambacho mchezaji anatakiwa kuwa nacho.
Kwa upande wa wanawake, Irene Kapambala (Polisi Stars), Tumwagile Joshua (DB Troncatti) na Amina Kaswa ni wachezaji tishio wanaongoza kwa kudaka mipira ya “rebound”.
Katika mzunguko wa kwanza Irene alikuwa anaongoza kwa kudaka mara 165, Tumwagile mara 157 na Amina Kaswa mara 142.