Tausi Royals, Pazi Queens tishio

WAKATI Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikizidi  kushika kasi, kwa upande wa timu ngeni katika ligi hiyo, Tausi Royals na Pazi Queens zinaendelea kuwa tishio kwa wakongwe zinazoshiriki  ligi hiyo.

Vitisho vya timu hizo inatokana na ushindi wa michezo miwili mfululizo waliopata katika mzunguko wa pili. 

Katika mchezo wa kwanza, Tausi Royals iliweza kuifunga Jeshi Stars kwa pointi 60-49 na mchezo wa pili ikaifunga Mchenga Queens kwa pointi 53-29.

Kwa upande wa Pazi Queens katika mchezo wa kwanza iliweza kuishinda DB Lioness kwa pointi 50- 49 na mchezo wa pili ikaifunga UDSM Queens kwa pointi 54-27.

Hadi sasa  timu ya Tausi Royals inashika  nafasi ya tatu  na Pazi Queens ikiwa ya sita, huku timu ya DB Troncatti ikiongoza kwa pointi 36  ikifuatiwa na Vijana Queens yenye pointi 34.

Kwa upande wa timu Tausi Royals imebakia kucheza na timu kongwe ya Vijana Queens, JKT Stars, DB Lioness na DB Troncatti.

Timu nyingine walizobakia kucheza nao ili wamalize mzunguko wa pili, ni Polisi Stars, Kurasini Divas, Mgulani Stars, Twalipo Queens, Ukonga Queens na City Queens

Upande wa Pazi Queens imebakia kucheza na Jeshi Stars, Vijana Queens na DB Troncatti, Kurasini Divas,  Ukonga Queens, City Queens, Polisi Stars, Mgulani Stars na Twalipo Queens.

Related Posts