KAMISHNA MKUU TRĄ AKUTANA NA WAFANYABIASHARA DODOMA

KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amekutana na kuzungumza na wafanyabiashara mkoani Dodoma. 

Akizungumza na wafanyabiashara hao Julai 24 mwaka huu, Kamishna Mwenda ameahidi kufanya kazi kwa ukaribu na wafanyabiashara hao pamoja na kutatua changamoto zao za kikodi kwa wakati ili kuleta ari ya ulipaji kodi wa hiari.

Wafanyabiashara hao wamemshukuru na kumpongeza Kamishna Mkuu huyo kwa kutenga muda wake na kuwasikiliza na kujenga ari ya kulipa kodi kwa hiari.

 

Related Posts