Na. Mwandishi Jeshi Dar es Salaam.
Fainali ya wiki ya nenda kwa Usalama kupigwa Julai 27,2024 katika viwanja vya chuo cha Taaluma ya Polisi DPA ambapo itawakutanisha timu kutoka jimbo la Kibamba na timu kutoka Jimbo la Segerea.
Akitoa taarifa ya fainali hiyo leo Julai 26,2024 mratibu wa Mashindano hayo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Muhidini Mpinga amesema mtanange huo utapigwa kesho kuanzia muda wa saa tisa alasiri katika Viwanja vya chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam.
Aidha Mpinga amebainisha kuwa katika fainaili hiyo elimu ya Usalama Barabarani itatolewa kabla na baada ya Mashindano hayo ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo endesha salama Ufike Salama.
Ameongeza kuwa kutokana na umahiri na umaarufu wa Mashindano hayo yaliyojichukulia sifa kubwa katika kuibua vipaji na kufikisha ujumbe kwa Jamii katika matumizi sahihi ya Barabara kutakuwepo burudani kutoka kwa wasanii wa hapa nchini.
Vile vile ametumia fursa hiyo kuwashukuru kampuni ya uuzaji wa pikipiki ya King Lion ambao wanauza pikipiki za mataili mawili na matatu.
Sambamba na hilo amewakaribisha wananchi katika viwanja vya Chuo Cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam ili kushuhudia mtanange huo wa kutaka nashoka ambao unawakutanisha vijana wa kabumbu kutoka Kipamba na Segerea.