AKATWA VIGANJA KISA WIVU WA MAPENZI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Rehema Paulo (26) Mkazi wa kata ya Katente iliyopo wilaya ya Bukombe mkoani Geita amejeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani na kukatwa viganja huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

 

 

Tukio hilo limetokea Julai 24, 2024 ambapo inadaiwa mwanamke huyo alikuwa na mgogoro wa kimapenzi na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Baba Law na kuwa siku ya tukio, alipigiwa simu na mtu wakaonane na alipofika, alivamiwa na kujeruhiwa.

 

 

“Nilipigiwa simu majira ya saa tano usiku na mwenyekiti maana mimi ni katibu wa balozi kwamba rehema amekatwa mapanga nikauliza rehema gani tena wakaniambia yule anayeuza sokoni amekatwa akiwa sokoni nikaamua nimpigie mwenyekiti tukaamua tupande bodaboda mpaka hospitali tukakuta kweli amelazwa hospitali hali yake ikiwa mbaya kwasababu amejeruhiwa kichwani na kukatwa mikono yote miwili” amesema Joyce Silenda ambaye ni Katibu wa balozi.

 

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa mkasa huo huku akisema kuwa hadi sasa mtuhumiwa na mke wake wametoroka na wanasakwa huku akiitaka jamii kupunguza roho za visasi.

 

 

Chanzo : East Africa TV

Related Posts