Na Khadija Kalili ,Michuzi Tv
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge leo amepokea hundi yenye thamani ya Mil.20 kutoka Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ikiwa ni katika muendelezo wa kuchangia watu wa Kibiti na Rufiji ambao wamepata changamoto ya mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea nchini kote.
Imeelezwa na Afisa Uhusiano wa TFS Johary Kachwamba kuwa msaada huo umetolewa na Kamishna wa Uhifadhi TFS ikiwa na lengo la kuwapa pole wakazi hao.
Afisa Uhusiano Kachambwa ndiye aliyemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge hundi hiyo ambapo makabidhiano yamefanyika katika viwaja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani.
“Wakaazi wa Kibiti na Rufiji ni wenzetu kwani tunazo hifadhi za misitu zaidi ya kumi zenye Hekta 32,000 hivyo ni wajibu wetu kuwapa pole” amesema Kachwamba.
“Tunatoa pole kwa RC Kunenge
Akizungumza mara baada ya kupokea hundi hiyo RC Kunenge ametoa shukrani zake za Mkoa kwa TFS dhati kwa hundi hiyo pia kwa kuwapa eneo ambalo watahamishiwa watu ambao wamepata chagamoto ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko katika maeneo ya Kibiti na Rufiji.
“Pia namshkuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa misaada ya hali na mali aliyowapatia wananchi wa maneo yaliyokumbwa na changamoto ya mafuriko ndani ya Mkoa wa Pwani ,Tunawashukuru TFS kwani fedha hizi zitasaidia kutatua changamoto zilizowakumba wenzetu wa KibitinaRufiji.