WANAOUGUA UGONJWA WA HOMA YA INI ASILIMIA KUBWA HAWAONI DALILI ZA MOJA KWA MOJA

Na Hadija Bagasha, Tanga.

WAKATI watanzania wakiadhimisha siku ya Homa ya Ini Duniani imeelezwa kwamba wagonjwa wanaougua ugonjwa huo asilimia kubwa hawaoni dalili za moja kwa moja isipokuwa asilimia ndogo.

Hayo yalibainishwa na Daktari wa Kituo cha Siha Polic Cliniki Kasanga Bashiru wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku hiyo ambapo wameazimisha kuwa kutoa vipimo bure kwa wananchi wa mkoa huo.

Alisema kwamba isipokuwa wanapata dalili ambazo ni kali kwa dalili ambazo sio za moja kwa moja ambazo zinaweza kufananishwa na magonjwa mengine kwa dalili ambazo ni viashiria vya moja kwa moja ikiwemo homa ya manjano kwenye sehemu za macho na mabadiliko ya ngozi mikono kubadilika rangi ya choo na kukosa hamu ya kula,

Aidha alisema kwamba athari za homa ya ini iwapo kwamba matibabu yake hayajafanyika itapelekea ini kushindwa kufanya kazi yake ya kawaida na kupelekea vifo huku akiitaka jamii kuona umuhimu wa kupata chanjo ya homa hiyo ili kuweza kukabiliana nao.

“Ndugu zangu leo wakati tunaadhimisha siku ya homa ya Ini Duniani ni vema kutoa wito kwa wananchi bado kuona umuhimu wa kujitokeza kupima na iwapo wakibainika kuwepo na ugonjwa huo waanza kuchukua hatua za kukabiliana nao”Alisema

“Kwa sababu mwamko wa wananchi kujitokeza kupima unasuasua lakini ukichukua takwimu kule walipotoka na wanapoelekea kwa kweli mwamko umeshaanza kuwa ni mzuri kwa siku ya leo mwamko umekuwa ni mzuri na hatua zinazoonekana kulingana na mwamko wa watu ni nzuri na hiyo ni kuendelea kupongeza juhudu mbalimbali ambazo zinafanywa na Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO)”Alisema

Akizungumzia umuhimu wa kuchanja homa ya ini alisema kuna umuhimu mkubwa kwa sababu ya takwimu zinaonyesha kwa magonwa makubwa ya matatizo ya ini asilimia 45 mpaka 50 yanatokana na homa za ini

“Hivyo umuhimu wa kuchanja ni kuhakikisha jamii inabaki salama bila kuwa na magonjwa hayo homa ya ini hapatis C,B kutokana na kwamba hatua za mwanzo haina dalili isipikuwa dalili zinajitokeza wakati ugonjwa umekuwa umefika mbali zaidi.

“Nitumie siku hii kuwahamasisha jamii ione umuhimu wa kuchanjo kwa maana iweze kujikinga na hapatatis B na C maana ni muhimu unapochanja hapatatis B uweze kujua na

Awali akizungumza Awadhi Abdul kutoka kwenye Kituo hicho alisema kwamba wao wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kufanyia watu vipimo vya homa aya ini na kutoa chanjo wao kama siha wanajitahidi kuhakikisha jamii inapata uelewa katika masuala ya kiafya lakini kutoa matibabu mbalimbali kwa jamii.

Aidha alisema kwamba ukiachia na homa ya ini wao wanatoa huduma mbalimbali za kimatibabu wana madaktari bingwa,huduma za maabara na huduma za mionzi mbalimbali, CT Scan na MRI kwa ghamara nafuu na zinazojali hali ya mtanzania.

“Tunashukuru kwa mwitikio ambao wameupata kwa jamii na lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanapiga vita homa ya ini kwa wananchi kwa kutoa elimu “Alisema

Naye kwa upande wake Daktari Jovin Amani alisema homa ina inathari kwa ujumla na dalili zake ni kujisikia kuchoka na viungo mkuu,kupata manjano,kupoteza fahamu au kutapika damu.

Hata hivyo aliwashauri watanzania waweze kujitokeza kupima ili kujua afya zao kwa ujumla maana homa ya ina imekaa sehemu kwa pamoja inaweza kuambukiza mtu yoyote inaweza kusambazwa kutoka mtu moja hadi mwengine.

Related Posts