Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wameendeleza ubabe katika mechi zao za kujiandaa na msimu ujao wa ligi Kuu ya NBC na mashindano ya kimataifa Kwa kuinyika Kaizer Chiefs mabao 4-0.
Mabao ya Yanga Kwenye mchezo huo yamefungwa na Prince Dube, Stephanie Ki Aziz aliyefunga mabao mawili na Clement Mzize.
Yanga wamekamilisha ziara yao chini Afrika Kusini ambapo ilishiriki michuano ya Mpumalanga Cup Kwa kucheza mechi Mbili, ikipoteza 2-1 Mbele ya Augsburg ya Ujerumani na Kisha ikashinda 1-0 dhidi ya TS Galaxy na Toyota Cup ambayo wameibuka mabingwa.