KESI YA KOMBO MBWANA DHIDI YA IGP, DPP YATAJWA KWA MARA YA KWANZA MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA

Na Oscar Assenga, TANGA

KESI ya Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kombo Twaha Mbwana dhidi ya Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP),Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC),Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) limetajwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga masijala ya Tanga chini ya Mh Jaji Happiness Ndesamburo.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Julai 17,2024 na mawakili 9 akiwemo Paul Kisabo kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),Peter Madeleka na mawakili wengine 7 ilifunguliwa katika mahakama hiyo kuomba kombo Mbwana akichiwe huru na kulipwa fidia kwa kushikiliwa kinyume cha sheria kwa takribani siku 29.

Katika uwasilishwaji wa shauri hilo, Kombo aliwakilishwa na Wakili Peter Madeleka na wakili Solomoni Kamunyu na upande wa utetezi wa wastakiwa umewakilishwa na Wakili wa Serikali Rashid Mohamed na hoja za msingi ziliwasilishwa mbele ya Mahakama kwa mujibu wa sheria.

Wakati wa kuwasilisha hoja za kila upande kuliibuka mkanganyiko kutokana na majina yaliyotajwa mahakamani hapo ambapo wakili wa Serikali alitaja jina la Kombo Mbwana Jumanne kama jina la mtu anayetajwa kwenye shauri hilo ambapo wakili Peter Madeleka akakana kuwa siyo jina la mteja wake kwani Jina la Mteja wake ni Kombo Twaha Mbwana.

Baada ya pande zote mbili kuwasilisha hoja zao mbele ya jaji Ndesemburo akasema amepokea hoja hizo na kuwa maamuzi ya shauri hilo yatatolewa Agosti 1, 2024

Akizungumza Wakili Madeleka alisema kwamba awali walifungua shauri hilo la mteja wao Kombo Mbwana Twaha Mahakama kuu Tanzania Kanda ya Tanga mbele ya jaji Happiness Ndesamburo ambalo liliharishwa kwa sababu Jaji alipata dharura na hakuwepo mahakamani hivyo likaitwa Julai 26, 2024.

Alisema katika kesi hiyo Kombo anawashtahiki Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (RPC),Mwanasheria Mkuu wa Serikali waende wakaieleze mahakama kwanini walimshikilia kinyume cha sheria kwa siku 29 na bado wanaendelea kumshikilia huko wanapomshikilia wao kwa siku zote ndio sababu kombo akaenda mahakamani hapo kupitia mawakili wake.

Alisema kwamba wanaiomba mahakama iweze kutoa maamuzi kama kombo anashikiliwa kihalali na kushikiliwa kwake kote huko kwa siku zote hizi ni kwa mujibu wa sheria na kama sio hivyo waliofanya hivyo wanatakiwa kufanywaje kwa mujibu wa sheria.

Alisema kwamba walipokuwa mbele ya Jaji wenzao walikuwepo upande wa wajibu maombi walikuwa na hoja kwamba shauri hilo liondolewe mbele ya Mahakam Kuu kwa sababu limepitwa na wakati kwa sababu kuna shauri lingine lipo Mahakama ya wilaya ya Tanga ambalo linahusisha Jamhuri dhidi ya mtu anaitwa Kombo Mbwana Jumanne hiyo ndio hoja yao kwamba shauri hilo liondolewe mahakamani.

Alisema kwamba wao waliwajibu kwamba shauri lilipo mahakamani linamuhusu Kombo Twaha Mbwana kama kuna shauri lolote lipo mahakama yoyote ya Tanzania linalomuhusu Kombo Mbwana Jumanne hilo shauri halimuhusu mteja wao na ndio maana bado wapo mahakamani kwa maana Jamhuri, IGP, RPC wanamshikilia mtu mwengine anaitwa Kombo Mbwana Jumanne.

Aidha alisema kwamba Kombo Twaha Mbwana hawajahi kuonekana tokea alipotoweka kwenye jamii na Jaji akalichukua hilo na wakamuambia aende akaangalia nyaraka zinasemaje kwa maana kwenye shauri hilo wao hawamuwakilishi Kombo Jumanne bali wanamuwakilisha Kombo Twaha Mbwana ambaye mpaka sasa hajulikani alipo.

“Huyo wanayesema yupo kwenye Gezereza la Maweni Tanga sio mteja wetu kwa sababu anaitwa Kombo Mbwana Jumanne kwa hiyo tofauti ya majina kisheria ni jambo kubwa na haliwezi kuchukuliwa kiutani mteja wetu tunamjua kwa chama,sura na mahusiano yake na watu wengine na sio ambaye wamemtaja mahakamani “Alisema Wakili Madeleka

Hata hivyo aliiambia kwamba shauri hilo ni halali lisikilizwee litolewe maamuzi lakini wenzao walikuja na ombi kama mahakama itakuwa na hoja ya kusikiliza shauri hilo wapewe siku 14 ili waweze kujibu hoja zilizowasilishwa na wao wakamuomba Jaji awape miezi miwili kwa sababu Kombo Mbwana ambaye ni kiongozi wa Chadema wilaya ya Handeni.

Alisema ni suala hilo ni kubwa sana na linahusu haki za binadamu na haki ya uhuru kuishi kama mtu huru haki ya kuonekana hana hatia hawezi kujibu hoja hizo kwa siku 14 hivyo wakaona kuna sababu ya kupewa miezi hiyo ili waweze wakaanaje majibu wao wayaleta waone kama yatakuwa yanakithi vigezo vya sheria.

Baada ya Jaji kusikiliza hoja zote mbili na licha ya kwamba ya kujua shtaka hilo limekuja kwenye hati ya dharura na lilihitaji kupewa atention ya haraka amesema atakuja kutoa uamuzi 1, Agosti 2024 kwamba kombo atapata dhamana au hawampi au kesi yake aliyoifungua mahakamani kuhusu IGP, RPC na wenzake inastahili kuendelea kuwepo mahakamani kama kesi halali.

Hata hivyo Wakili Madeleka alisisitiza kwamba kuna utamaduni ambao umejengeka na kuaminiana kwamba mtu akishikiliwa na Polisi kinyume cha sheria kwa siku kadhaa halafu akaamua kupitia mawakili wake kupeleka shauri aombe aletewe mahakamani halafu kule wakamuachia eti shauri lake lililoletwa Mahakama Kuu litakuwa limekufa.

“Niwaambie kwamba litakuwa halijafa halijafa lengo la mashauri kama hayo ambayo kombo amefungua ni la kutaka pamoja na mambo mengine wajibu maombi waeleze mahakama walikuwa na uhalali gani wa kukakaa na mtu siku zote hizo kwa sababu ukishampata hawawezi kumuachi Jaji na kuondoka hapana wanapaswa kumleta na kumueleze wanalikuwa wanamshikilia kwa sababu gani…suala hili bado ni bichi mnoo kama maharage ya mbeya ambayo yanahitaji muda sana kuiva “Alisisitiza.

Related Posts