Kinana ajiuzulu CCM, Samia aridhia

Dar es salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amejiuzulu wadhifa huo baada ya kuomba mara kadhaa kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan ambaye sasa ameridhia ombi hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Julai 29, 2024 na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makala imesema Kinana ameandika barua ya kuomba kupumzika.

Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM Samia amesema: “Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya makamu mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda mfupi kama ulivyoomba, na kwa kweli nilipenda uendelee kutusaidia lakini kwa kuwa umeomba sana na ahadi ni deni nalazimika kwa moyo mzito kuridhia kujiuzulu kwako.”

Rais Samia amesisitiza kuwa Chama kitaendelea kutumia uzoefu na maarifa ya Kinana kila itakapohitajika.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts