Shambulio la Kisu Katika Tamasha la Watoto laacha Vifo na Majeruhi – MWANAHARAKATI MZALENDO

Katika tukio la kutisha lililovuruga utulivu wa jiji la Southport, watoto wawili walipoteza maisha na wengine tisa kujeruhiwa vibaya, sita kati yao wakiwa katika hali mbaya baada ya shambulio la kisu katika warsha ya watoto iliyokuwa ikiendesha mafunzo ya densi.

Katika harakati za kuwalinda watoto katika hafla hiyo iliyokuwa ikiitwa Taylor Swift, iliyofanyika kwenye Mtaa wa Hart, Southport, watu wazima wawili walijeruhiwa vibaya na sasa wapo katika hali mahututi, Polisi wa Merseyside walithibitisha.

Kijana mwenye umri wa miaka 17 kutoka Banks, Lancashire, amekamatwa na anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji na jaribio la kuua, huku polisi wakijaribu kufahamu sababu ya shambulio hilo, ingawa wameweka wazi kuwa halina uhusiano na ugaidi.

Shuhuda mmoja alielezea tukio hilo kama “la kutisha” na kusema “hawajawahi kushuhudia kitu kama hicho maishani mwao.”

Mfalme na Waziri Mkuu waliongoza kutoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na kwa wale walioathiriwa na tukio hili la kusikitisha.

Polisi wa Merseyside walitangaza kuwa tukio kubwa limetokea baada ya kupokea simu za dharura saa 11:47 jioni, wiki ya kwanza ya likizo za shule wakati wa majira ya joto kwa watoto wengi nchini Uingereza.

Magari ya polisi, ambulensi 13, na magari ya zimamoto yalifika haraka eneo la tukio ambapo tamasha la watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 10 lilikuwa likifanyika, huku juhudi za kuwaokoa na kuwahudumia majeruhi zikiendelea kwa kasi kubwa

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts