FAHAMU KUHUSU SHERIA YA ARDHI TANZANIA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Kiujumla hamna mtu mwenye umiliki kamili wa ardhi Tanzania, na badala yake, Rais ndo mwenye umiliki kamili wa Ardhi ambaye yeye ni kama Muaminifu (Trustee) wa ardhi yetu kama inavyoelezwa chini ya kifungu cha 3(1) (a) cha Sheria ya Ardhi.ImageLakini pia hapohapo, ardhi tunayoruhusiwa kumiliki ni yote isipokuwa ardhi yenye madini na mafuta kama ilivyoelezwa chini ya kifungu cha 2 cha Sheria ya Ardhi.ImageSheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu cha 20,inatoa katazo kwa mtu ambae sio raia wa Tanzania kumiliki ardhi.

Sheria inatoa mwanya kwa wawekezaji pekee kuweza kutumia ardhi kupitia uwekezaji ambapo ardhi hutolewa kwao kwa matumizi ya uwekezaji tu na sio shughuli nyingine

Muwekezaji huyo atafanya maombi ya umiliki wa ardhi kwa njia ya uwekezaji kupitia TIC (Tanzania Investment Center- Kituo cha Uwekezaji Tanzania) ambayo ipo kisheria chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania.

(kifungu cha 17 kifungu kidogo cha 7 cha Sheria ya Uwekezaji Sheria Na. 26 ya mwaka 1997).ImageNa umiliki huo wa ardhi kwa ajili ya uwekezaji hautozidi miaka 99 kama ilivyoelezwa chini ya kifungu cha 22(2) cha Sheria ya Ardhi Sura ya 113.

Maoni ayko ni yapi juu ya nini kirekebishwe ndani ya hii sheria ya Ardhi?

Chanzo; Maabara ya Sheria (Mtandao X).

#KonceptTvUpdates

Related Posts