Kufuatia maandalizi ya Kombe la Dunia 2034, nchi mbalimbali zimekuwa zikituma maombi ya kugombea kuhodhi mashindano hayo, makubwa zaidi duniani katika mchezo wa mpira wa miguu.
Siku ya Jumatatu, Saudi Arabia iliwasilisha rasmi nia yake ya kuandaa Kombe la Dunia la 2034 mjini Paris, katika hafla iliyoandaliwa na FIFA. Ujumbe wa Saudia uliongozwa na Mwanamfalme Abdulaziz bin Turki bin Faisal, Waziri wa Michezo, pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka la Saudia, Yasser Al-Meshal, na watoto wawili kutoka vituo vya mafunzo vya Chama cha Soka cha Saudi Arabia.
Waziri wa Michezo wa Saudia alielezea kuwa stakabadhi hizo zinaonyesha maono ya taifa kuelekea mustakabali mzuri na kuonyesha nia ya Ufalme wa kuandaa tukio kubwa zaidi katika ulimwengu wa soka, huku ikithibitisha nafasi ya Saudia kwenye ramani ya dunia katika nyanja mbalimbali, ikiwemo michezo.
#KonceptTvUpdates