Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
ALIYEKUWA Meya wa Ubungo Dar es Salaam, Boniface Jacob na mwenzake Godlisten Malisa, ambaye ni Afisa Afya Jamii na mkazi wa Moshi, Kilimanjaro leo Julai 30,2024 wamesomewa maelezo dhidi ya shtaka lao la kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, washtakiwa hao waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu Kisutu, walikana kuchapisha taarifa hizo na kukubali taarifa zao binafsi tu.
Hata hivyo mapema, kabla ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema akisaidiana na Neem Mushi aliiomba mahakama kufanyia marekebisho hati ya mashtaka jambo ambalo Mahakama ilikubali
Akisoma maelezo hayo, Mrema alidai Aprili 22, 2024 Jacob akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alichapisha taarifa ya uongo kupitia mtando wake wa kijamii wa X wenye jina la Boniface Jacob wenye kichwa kilichosomeka ‘Wenye leseni ya kuua wameua Tena’.
Taarifa hiyo ilieleza ‘kijana wetu Rajabu Mlanga Mushi maarufu kama Babu G, amekutwa Hospitali ya Kilwa Road akiwa ameuwawa. Imagine tumetoa taarifa Jeshi la polisi la kupotelewa kwa kijana wetu , cha ajabu Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam likawa linatusaidia kumtafuta pia’
‘Kila siku jeshi la polisi linasema halijapata taarifa wala fununu zozote za kijana wetu na kwamba tuwe wavumilivu wanapambana kuendelea kumtafuta .Jana machale yakawacheza ndugu wa kijana baada ya msiri mmoja kuwatonya ndugu ‘nendeni hospitali ya polisi Kilwa road mkachungulie vyumba vya kuhifadhia maiti’.
‘Ndugu walivyokwenda huko hospitali ya polisi Kilwa road wakamkuta kijana wao akiwa ameuwawa, wahusika wa hospitali wanadai maiti ililetwa tangu tarehe 10 Aprili mwaka 2024, na na askari wa Jeshi la polisi’.
‘Wacha wanyonge tukazike maiti zetu, sitamani hata kuona ndugu wakiomba uchunguzi dhidi ya maiti yao kwasababu hata mtoto mdogo anajua hapo Muuaji ni nani’,
‘Pili tunajua ile mbinu ya ‘TAPE’, ile kufunga mtu miguu, kufunga mikono kisha kupigwa tape ya mdomo na puani hadi kifo baada ya ile mbinu ya kupeleka msituni ,porini na kupigwa risasi kujulikana. Dar es Salaam ina mtu mmoja katili sana’.
Alidai kuwa Machi 19, 2024 Jacob akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alichapisha taarifa ya uongo kupitia kompyuta mpakato wenye jina la X , kwa jina la Boniface Jacob @ExMayorUbungo wenye kichwa kisomekacho ‘ Mauaji Arusha’.
Ilidaiwa kwamba taarifa hiyo ilisomeka ‘Mwananchi mwenzetu na aliyekuwa dereva wa magari ya watalii Omary Msamo ameuwawa na skari wa Jeshi la polisi wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha’.
Omary Msamo ameuwawa baada ya kusimamishwa na kushushiwa kipigo kizito kilichopelekea kutoa uhai wake na polisi wa usalama barabarani baada ya kutuhumiwa kuendesha gari akiwa ametumia kilevi’.
‘Kwamba, jeshi la polisi linatumia kila jitihada kuzuia vyombo vya habari kuripoti tukio hili kama nia ya kuficha na kuwanusuru askari wake dhidi ya mkono wa sheria’ .
Alidai kuwa, Aprili 22, mwaka huu ndani ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ,kwa lengo la kupotosha umma , alichapisha taarifa za uongo kupitia kompyuta mpakato, kwenye akaunti yake mtandao wa kijamii wa Instagram ya jina la Malisa_gj.
Taarifa hiyo ilisomeka kwamba ‘Aprili 13 Meya mstaafu wa Manispaa ya Ubungo @exmayor_bonifacejacob alitoa taarifa ya kupotelewa na ndugu yake Bw. Robert Mushi maarufu kama Babu G, ambaye alipote mapema mwezi Aprili 2024’.
‘Inadaiwa alikamatwa na watu waliojitambulisha kuwa polisi maeneo ya Kariakoo na baada ya hapo hakuonekana tena’.
‘Leo wakaambiwa nendeni hospitali ya polisi Kilwa road ndugu yenu amefichwa monchwari pale
wakaenda. Lahaula!, wakamkuta Robert akiwa katika jokofu la baridi, hakuwa Robert tena bali mwili wake ukiwa na majeraha ya kipigo’ .
Wakili Mrema amedai kuwa upelelezi ulifanyika na washtakiwa wakabainika kuwa walitenda makosa hayo ndipo kesi ilipofunguliwa na walipokamatwa na kupekuliwa walikutwa na laptop, simu na laini za zingine.
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Agosti 29, 2024. Washtakiwa wote wako nje kwa dhaman