Mwalimu mbaroni kwa tuhuma za kumlawiti mtoto darasa la pili

Tabora.  Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia mwalimu mmoja (jina limehifadhiwa) wa Shule ya Awali ya St. Doroth iliyopo Manispaa ya Tabora kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa shule hiyo anayesoma darasa na pili.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Julai 30, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tayari wanamshikilia mwalimu huyo kwa mahojiano.

Amesema uchunguzi ukikamilika, mwalimu huyo atafikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi ikiwamo kufikishwa mahakamani.

“Mnamo Julai 25 mwaka huu saa 3:45 usiku, mama mmoja mkazi wa Cheyo aligundua kulawitiwa kwa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la pili chanzo kikiwa ni tamaa za kingono kwa mwalimu,” amesema kamanda huyo.

 “Baada ya kupata taarifa hizo tuliweka mtego na kufanikiwa kumkamata mwalimu wa shule hiyo na baada ya mahojiano, tuligundua alikuwa anatumia mbinu za kumuingiza mtoto kwenye vyoo vya shule na kumfanyia ukatili huo na mpaka sasa tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi.”

Hata hivyo, Kamanda Abwao amedai uchunguzi wa daktari umethibitisha mtoto huyo kuingiliwa kinyume na maumbile.

Akizungumzia tukio hilo, Mchungaji wa Kanisa la EAGT Kidatu B, Rashid Jumanne amesema kuendelea kutendeka kwa matendo ya kinyume na maagizo ya Mungu, kunatokana na watu kutokuwa na hofu ya Mungu.

“Wakati mwingine imani za kishirikina zinawafanya watu wafanye matendo ambayo ni kinyume na matakwa ya Mungu hivyo, mamlaka zina wajibu wa kuhakikisha matendo haya yanatokomea, lakini pia hata sisi viongozi wa dini, tutaendelea kuongea na waumini wetu ili kuona wanavyoweza kuacha matendo hayo,” amesema mchungaji huyo.

Kanani Chombara ni Wakili Manispaa ya Tabora amesema matendo ya ulawiti yamekatazwa kisheria na yana madhara makubwa kwenye jamii.

Related Posts