SABABU KIFO CHA ISMAIL HANIYEH – MWANAHARAKATI MZALENDO

Taarifa iliyotolewa mapema Jumatano asubuhi, Hamas ilithibitisha kwamba Ismail Haniyeh aliuawa katika uvamizi wa Israel alipokuwa ziarani Tehran kwa ajili ya kuapishwa kwa Rais Masoud Pezeshkian. Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran pia limethibitisha kifo chake, huku Israel na viongozi wake wakubwa wakiwa hawajatoa majibu rasmi kuhusu madai haya. Kifo cha Haniyeh, ambaye alikuwa kiongozi muhimu wa Hamas akiwa uhamishoni nchini Qatar, kimeacha pengo pigo kubwa kwa kundi la Palestina.

Kifo hiki kinakuja saa chache baada ya Israel kushambulia kamanda mkuu wa Hezbollah mjini Beirut, kufuatia shambulio la roketi lililoshambulia milima ya Golan na kusababisha vifo vya watu 12. Mashambulizi haya ya hivi karibuni yanazidisha wasiwasi kuhusu mzozo wa kieneo.

Afisa wa Hamas ametishia kulipiza kisasi kwa mauaji ya Haniyeh, akisema ni “kitendo cha kioga.” Israel, kwa upande wake, imekuwa ikitishia kuangamiza viongozi wa Hamas baada ya uvamizi wa Oktoba 7, ambao ulisababisha vifo vya watu 1,200 na kuchukua mamia ya mateka.

Kutokana na migorogoro ambayo imekuwa ikijirudia rudia katika ukanda huu wa nchi za kiarabu, ambayo mara nyingi vyanzo vyake vikiripotiwa kuwa ni mzozo wa kieneo, watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha, kulamika kuhama makazi yao na kukosa na kukatishwa kwa hudma za kijamii.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts