Tunachunguza vifaa vilivyopokelewa na havionekani hospitali ya Katoro wilaya ya Geita

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Geita imeanza kuchunguza Upotevu wa Baadhi ya Vifaa vilivyonunuliwa na kupokelewa katika Hospitali ya Katoro ambapo vifaa hivyo vimeonekana kupokelewa lakini havionekani wala kutumika sanjali na kutoonekana katika stoo.

Hayo yameelezwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita , Alex Mpemba wakati akitoa taarifa ya kipindi Cha April hadi Juni 2024 Ofisini kwake ambapo amesema TAKUKURU Imebaini upotevu huo katika ujenzi wa Hospitali ya katoro awamu ya Pili wenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.7.

Mpemba amesema wamebaini Miradi miwili ya Afya yenye thamani ya Shilingi 1,727,000,000 ambayo matumizi ya Fedha katika utekelezaji wa miradi hiyo ina mapungufu na kuwalazimu kuanzisha uchunguzi .

Aidha Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Geita TAKUKURU imesema itaendelea kuwashirikisha wadau wote katika kudhibiti rushwa kuanzia kipindi hiki cha Mchakato wa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Related Posts