Chelsea wamekamilisha uhamisho wa Jörgensen

Chelsea wamekamilisha usajili wa mlinda mlango wa Denmark chini ya umri wa miaka 21 Filip Jörgensen kutoka Villarreal ya LaLiga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye msimu uliopita alikua kipa nambari 1 wa Villarreal, amesaini mkataba wa miaka saba, Chelsea ilisema.

Vilabu havikufichua ada ya uhamisho lakini vyombo vya habari vya Uingereza viliripoti kuwa dili hilo lilikuwa na thamani ya takriban £20m.

Related Posts