Gari yako ikigoma kuwaka usikurupuke, angalia maeneo haya matano

Gari ni mashine iliyotengenezwa na binadamu hivyo hata kama unalithamini kiasi gani ugonjwa hutokea tena bila hodi na ndiyo maana ukiwa na gari unatakiwa ujiandae kwa lolote litalotokea.

Mojawapo ya matatizo ya gari ni kusumbua kuwaka yaani kiufupi hata kama umetoka kulinunua karibuni, tatizo hili linaweza kutokea na inaweza kuwa kubwa au dogo.

Leo tutaangalia sababu kadhaa ambazo zinasababisha gari lishindwe au lisumbue kuwaka au endapo likikutokea tu basi angalia haya mambo kwanza kabla hujafikiria vinginevyo.

Kulegea kwa terminal za betri

Hii ni sababu kubwa ambayo inapelekea gari kushindwa kuwaka. Kumbuka betri ndiyo chanzo kikuu cha umeme kwenye gari lakini pia ndiyo chanzo cha dharura cha umeme hivyo hata kama gari ni jipya kama betri ni mbovu basi jua hiyo ni changamoto.

Hakikisha unapofanya shughuli inayohusu betri basi unairudishia na kuikaza inavyotakiwa kwani ikilegea kidogo inaweza kusababisha kutotoa volt husika za kufanya gari liwake.

Nitajuaje shida ni betri? Endapo unawasha na starter haizungushi yaani hailiii ule mlio wa kuwasha gari basi jua shida inaweza kuwa ni betri na mara nyingi huleta mlio wa “triiiiiii triiiii” basi hebu kagua betri kwanza.

Gari ili liwake linahitaji mafuta ya kutosha, hivyo yanapokuwa machache pampu inakosa cha kupeleka na injini kukosa kitu cha kuchoma hivyo gari halitoweza kuwaka. Tofauti yake na sababu ya betri ni kwamba hapa gari itakuwa starter inazungusha lakini haiwezi kupokewa na injini.

Kazi ya starter ni kupeleka mshindo kwenye injini ili iweze kuruhusu piston zifanye kazi yake na hatua nyingine zifuate mpaka kupelekea gari kuwaka. Kwa lugha nyingine, starter ni switch ya kuruhusu injini iwake hivyo inapokuwa mbovu basi gari halitawaka.

Starter nyingi ugonjwa huanza taratibu sasa kumbuka njia pekee ya kutibu ni kuipeleka kwa fundi itengenezwe au ununue mpya.

Kuharibika kwa switch ya stata

Hapa tunaongelea ile sehemu ya kuingiza funguo na kuwasha gari. Kutokana na matumizi yake kuwa ni ya mara kwa mara huwa inatokea switch hii kuharibika na pindi inapoharibika hutoweza kuwasha gari na suluhisho kubwa la tatizo hili ni kubadilisha tu switch na kuweka nyingine.

Endapo utaigusa na kuhisi joto kali kwenye switch basi jua kutakuwa na tatizo kwenye wiring yake kwenye hivyo unahitaji fundi umeme kuifuatilia.

Fuse imetengenezwa kukata endapo kutakuwa na kuongezeka kwa nguvu ya umeme au kama kutakuwa na shida ya kiumeme ya kifaa husika ambacho kinalindwa na fuse hiyo na ndiyo maana kunakuwa na fuse nyingi sana kwenye fusebox ya gari yako na kila fuse ina kifaa chake inalinda

Hivyo endapo fuse ya labda ya pampu ya mafuta imekata basi jua pampu hiyo haitafanya kazi na kama haitafanya kazi basi jua mafuta hayatapelekwa kwenye injini na gari halitawaka.

Related Posts