Timu ya Tabora United imefanikiwa kuinasa saini ya kocha mkenya, Francis Kimanzi aliyewahi kuitumikia timu ya Tusker ya Kenya na timu ya Taifa ya Kenya kuwa kama kocha mkuu wa timu hiyo kuelekea msimu mpya wa ligi kuu NBC.
Kufuatia na kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Mrundi Masoud Juma, aliyeondoka siku chache kabla ya marudiano ya mchezo wamchujo (play off), Tabora United imefikia makubaliano na kocha Franscis Kimanzi ambaye ameshatua katika viunga vya Tabora United akisubiri kutambulishwa ramsi.
Huku mmoja ya vigogo wa Tabora United alinukuliwa akisema “Tutakuwa na Kimanzi bodi ya klabu yetu imeona ndiye kocha anayetufaa. Nadhani wiki hii ataanza kazi, amebakiza kuja tu nchini”, wakati huo ameuagiza uongozi wa Tabora United kuipeleka timu Dar es salaam kwa ajli ya kuendelea na maandalizi ya msimu ujao.
“Tulikuwa tunatafuta kocha mwenye uzoefu kidogo na soka la Afrika na Kimanzi ni miongoni mwa makocha bora Afrika Mashariki” aliongeza.
@KonceptTvUpdates