Tanzania, Malawi na Msumbiji waingia makubaliano mto Ruvuma

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso waziri mwenyeji wa umoja wa nchi tatu zinazonufaika na Mto Ruvuma Tanzania, Malawi na Mozambique ameongeza Mkutano na Hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za maji za Mto Ruvuma kwa nchi za Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Mkutano huu umehudhuriwa na Waheshimiwa wa Maji wa nchi hizi tatu Waziri wa Maji Tanzania Mhe Jumaa Aweso mwenyeji, Mhe Abida Sidik Mia Waziri wa Maji Malawi, na Mhe Carlos Mesquita Waziri wa Maji Msumbiji Leo tarehe 31 Julai 2024 Four Points by Sheraton Hotel Dar Es Salaam Tanzania.

Wakizungumza katika nyakati tofauti Mawaziri wa Maji wa nchi hizi tatu wamesema usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji hususani mto Ruvuma ni kipaumbele cha viongozi wakuu wa nchi zao.

Aidha Waziri Aweso akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano amesema amewasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambae katika nyakati tofauti amesisitiza na kuhamasisha mashirikiano mema katika utunzaji na uendelezaji wa Rasilimali za Maji.

Related Posts