Timu ya wanawake ya Simba Queens imemtambulisha kiungo wao mpya mshambuliaji ambaye ni raia wa Nigeria Precious Christopher akitokea timu ya Wanawake ya Yanga Princess.
Pia timu hiyo imekamilisha sajili nyingine mbili za wachezaji kutoka Yanga Princess akiwemo Saiki Atinuke raia wa Kenya pamoja na Wincate kaari raia wa Nigeria.
Hadi sasa timu hiyo imekalisha sajili za wachezaji sita kuelekea msimu ujao wa ligi ya wanawake pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.