SPOTI DOKTA: Kimbia ukate mafuta mwilini

KUMEKUWAPO na matukio mbalimbali ya mbio za hisani, ambayo yamekuwa yakitumika kuhamasisha mazoezi kama nyen-zo ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza maarufu kitabibu kama NCD.

Katika mbio nyingi viongozi wa serikali, wakuu wa taasisi mbalimbali toka serikalini na binafsi wamekuwa wakionyesha mfano wa umuhimu wa mazoezi kwa jamii ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

Mwanaspoti Dokta ikiwa ni mdau wa afya na mazoezi inaunga mkono juhudi za kukata mafuta ili kujenga afya kwa na hivi karibuni ilishiriki moja kwa moja katika mbio za kilomita 10.

Kadri inavyojiandaa na kufanya zoezi la kukimbia mara kwa mara inasaidia mwili kuweza kujishughulisha na hatimaye kutumia mafuta yaliyorundikana mwilini kama akiba ya matumizi inapohitajika.

Unapokimbia zaidi ndivyo pia unatumia akiba ya nishati ya mwili iliyorundikiwa hatimaye kukusaidia kukata mafuta. Uwepo wa mafuta mwilini ndio chanzo cha magonjwa yasiyoambukiza NCDs ikiwamo ya moyo na mishipa, kisukari, kiha-rusi na figo.

Ukimbiaji mdogomdogo hujulikana kama jogging huanishwa kama moja ya zoezi jepesi yaani aerobic exercise ambayo mtu yeyote mwenye uhitaji wa mazoezi kwa ajili ya utimamu wa afya ya mwili anapaswa kufanya.

Kutokana na upigaji hatua za maendeleo katika nchi yetu vivyo hivyo kunaendana na kuongezeka kwa visa vya ma-gonjwa yasiyoambukiza kitabibu yakiitwa Non Communicable Diseases (NCDs).

Magonjwa yanatokana na mienendo na mitindo mibaya ya kimaisha ikiwamo kutoushughulisha mwili na mazoezi na ulaji holela wa vyakula hatimaye jamii hukumbwa na tatizo la unene au mafuta.

Mwamko wa ukimbiaji unatokana na ukweli kuwa jamii imeanza kutambua kuwa zoezi la kukimbia kidogo kidogo ni nyenzo muhimu katika kukabiliana na unene ambao ndio futa lilorundikana mwilini.

Tafiti zinathibitisha kwamba zoezi linalochangia watu kuwa na utimamu bora wa afya ya mwili na kuishi muda mrefu ni  la kukimbia kidogokidogo kwani linawezesha mwili kukata futa.

Uwepo wa futa yaani unene humuweka mtu katika hatari zaidi ya kupata magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya mishipa ya damu, kiharusi, ugonjwa sugu wa figo na saratani.

Kwa kutambua hilo taasisi nyingin zimeamua kutumia njia hii kuhamasisha jamii kushiriki mazoezi kama njia rahisi ya kukata futa hatimaye kujenga afya bora.

UKIMBIAJI UNAVYOKATA FUTA

Mazoezi mepesi ya kukimbia na kutembea kwa kasi ya wastani yanasaidia kuufanya mwili kushughulisha viungo vingi hivyo kuchoma mafuta yaliyorundikana ikiwamo katika eneo la kitambi.

Lakini inashauriwa ili kuweza kuchoma mafuta ya ziada ni pale utakafanya mazoezi mepesi kwa muda wa dakika 30-60 kuendelea.

Katika mbio hizo kulikuwa na mbio za kilomita 5, 10, 21 na 42. Mshiriki akitumia muda wake vizuri tangu maandalizi ya mapema anaweza kunufaika na mbio hizo kukata futa.

Ni muhimu kabla ya mazoezi yoyote lazima mwili uandaliwe kwa mazoezi ya viungo kwanza ili kuuweka utayari wa viun-go kufanya mazoezi kwa ufanisi.

Zoezi la kukimbia ni zoezi zuri ambalo linaweza kuwafaa vijana zaidi. Watu wazima pengine kukimbia ni changamoto wanaweza kufanya zoezi la kutembea lakini kwa mtindo wa kutupa mikono kama vile watembeavyo askari. Mtindo huo hu-saidia kushughulisha maeneo mengi ya mwili ikiwamo misuli ya eneo la tumboni.

Ili kuleta matokeo chanya zaidi katika ukimbiaji ili kukata futa unaweza kuchanganywa na mazoezi ya viungo ambayo yanalenga kuishughulisha misuli ya tumboni.

Pia tumia mbinu ya kutumia muda mwingi na mara kwa kwa kukaza misuli yako ya tumbo hata unapokuwa katika kazi za-ko za kila siku inasaidia kuishughulisha misuli ya tumbo.

Unaweza kutumia dakika 30-60 kufanya mazoezi mepesi na dakika 10 ya moja kwa moja ya tumboni. Baada ya mazoezi yoyote ni muhimu pia kutumia dakika tano za mazoezi ya kuupoza.

Kumbuka kuwa kitambi ni ishara ya uwepo futa jingi hivyo kuwa katika hatari ya magonjwa yasiyoambukiza, fika katika huduma za afya kwa ushauri zaidi.

Ni vizuri kumuona daktari kabla ya kuamua kuanza programu ya mazoezi ya ukimbiaji ili kufanya uchunguzi wa jumla wa mwili kabla ya kuanza kufanya mazoezi haya.

Uchunguzi huu unaweza kubaini matatizo ya afya yanayoweza kuwa kikwazo na pia kubaini dosari za kimwili ikiwamo unyayobapa au matatizo ya maungio ya mwili.

Inawezekana umri wako ni zaidi ya 40+, una unene uliokithiri au haujawahi kufanya mazoezi kwa muda mrefu. Kuanza ghafla mazoezi ya ukimbiaji inaweza kuleta changamoto za kiafya ikiwamo kupumua kwa shida, kuhisi kuchoka kirahisi na maumivu ya mwili.

Kukimbia hakufanywi kiholela tu, lazima kujua je una uzito kiasi gani? Kukokotoa zao la uwiano wa uzito (KG) gawa kwa urefu wa mwili (M xM) katika mita kipeuo cha pili, hujulikana kama Body Mass Index –BMI ni nyenzo rahisi ya kutathimini uzito.

Ni muhimu kufanya mazoezi ya ukimbiaji kuendane na lishe unayokula kwani mazoezi yenyewe yanaongeza hamu ya ku-la. Kama unafanya mazoezi ili kukata futa ni vizuri kupata ushauri wa wataalam wa lishe za wanamichezo.

Vyakula vyenye wanga nyingi, mafuta mengi na sukari nyingi ni muhimu kuepukwa kwa yule ambaye anafanya mazoezi ili kukata futa hatimaye kudhibiti uzito wa mwili.

Ushiriki mathon mara kwa mara inakupa hamasa ya kushiriki ukimbiaji hatimaye kusaidia kukata futa mwilini hivyo kuleta mato-keo makubwa katika kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza (NCD). Endelea kushiriki marathoni zijazo ili kuendelea kukata futa zaidi.

Related Posts