UVCCM ni kiunganishi cha vijana

Katibu Mkuu wa Uvccm Jokate Mwegelo amekagua Uwanja wa New Amaan Complez Kuelekea Kampeni ya kijana na Kijani ambayo mgeni Rasmini anatarajiwa kua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Baada ya kuizindua Kampeni hiyo upande wa Tanzania Bara katika Uwanja wa Mkapa Studium

Kampeni hiyo ya Kijana ni Kijani imelenga kuwaunganisha vijana kwa kuibua vipaji na kuwakutanisha na viongozi wao na kutoa fursa mbali mbali na itafanyika siku mbili kabla ya siku ya Vijana Duniani

Jokate amesema kampeni hiyo inatarajiwa Kuzinduliwa tarehe Kumi Mwezi wa nane siku ambayo imepewa jina la siku ya Kijana inayokwenda sambamba na siku ya Vijana Duniani ambayo huazimishwa Tarehe kumi na Mbili ya Mwezi wa Nane jokate amesema umoja wa Vijana Ccm ni kiunganishi wa Vijana wote wa Tanzania bila ya kuwabagua kwa kazi wanazozifanya.

 

Related Posts