RAYVANNY AIBUKIA DEEDS MAGAINE – MWANAHARAKATI MZALENDO

Muziki wa Tanzania unaendelea kuvuma kimataifa kupitia juhudi za wasanii wa Bongofleva, ambapo Rayvanny, staa wa Next Level Music, amejipatia nafasi ya kuonekana kwenye jarida maarufu la Afrika, ‘Deeds Magazine.’ Jarida hili linaangazia vipaji na ubunifu kutoka Nigeria na Afrika kwa ujumla.

‘Deeds Magazine,’ imemtaja Rayvanny kama Msanii bora wa kidijitali, akieleza maono yake ya kimataifa na jinsi anavyotaka kukuza vipaji vipya. Amefafanua safari yake ya kutoka mitaani hadi kumiliki lebo ya muziki, akionyesha azma yake ya kufanikiwa kimataifa na kuleta tuzo nyumbani.

Rayvanny amesema anaona mbali zaidi ya muziki wa Afrika Mashariki na ana nia ya kulitawala soko la muziki wa kimataifa kwa manufaa ya Watanzania na dunia kwa ujumla.

Hii ni njia nyingine muhimu kwa Rayvanny na wasanii wengine wa kizazi kipya wa Tanzania, ambao wanapanua wigo wao kimataifa kwa kujihusisha na matukio mbalimbali na kushirikiana na majarida na vyombo vya habari vya kimataifa. Mafanikio haya yanasaidia kueneza sanaa ya Tanzania ulimwenguni na kuonyesha kuwa muziki wa Tanzania unaweza kufanikiwa katika soko la kimataifa kwa ubunifu na ubora wake.

 

#KonceptTvUpdates

Related Posts