Kiongozi wa Sudan al-Burhan anusurika shambulizi la droni – DW – 31.07.2024

Shambulizi hilo la droni liliilenga kambi moja ya kijeshi iliyoko mashariki mwa Sudan wakati wa ziara ya mkuu wa majeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na kuzidisha wasiwasi kuhusu mustakabali wa juhudi za hivi karibuni za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 15. Jeshi la Sudan laapa kulipiza kisasi shambulizi la RSF lililoua watu 100

Taarifa ya jeshi la Sudan imesema kuwa shambulizi hilo limetokea wakati wa mahafali katika kambi ya kijeshi ya Gibeit iliyoko kilometa takribani 100 kutoka mji mkuu wa kijeshi wa Port Sudan. Maafisa kutoka serikalini, ambayo inaungwa mkono na jeshi walisema kuwa kiongozi huyo yuko salama na amepelekwa Port Sudan.  Burhan ametoa kauli baadae akisema kwamba

“Hatutarudi nyuma, hatutasalimu amri na hatutajadiliana na mtu yeyote. Hakuna kinachotutisha hofu, hakuna droni itakayotutisha hadi tufe.”

Sudan Darfur El Fasher
Sudan Darfur El FasherPicha: AFP

Vidio iliyosambaa kupitia mitandao ya kijamii na kuthibitishwa na shirika la habari la Reuters, imewaonyesha wanajeshi wakipiga gwaride katika sherehe za mahafali kabla ya sauti ya kishindo kusikika ikifuatiwa na mlipuko. Vidio nyingine ilionyesha wingu zito la vumbi na watu wakikimbia. Shirika la Human Rights Watch lalishtumu kundi la wanamgambo wa RSF kwa dhulma za kingono dhidi ya wanawake

Afisa mmoja wa RSF ambaye ni mshauri wa kisheria Mohamed al-Mukhtar amesema mashambulizi hayo huenda yamefanywa na Waislamu wenye itikadi kali. Ameongeza kuwa RSF haina uhusiano wowote na ndege zisizo na rubani na hayo ni matokeo ya mgawanyiko wa ndani kati ya Waislamu.

Soma: Daglo akaribisha mazungumzo ya kusitisha mapigano Sudan

Shambulio hilo la Droni ni la hivi karibuni katika mkururo wa mashambulizi kama hayo dhidi ya maeneo ya kijeshi karibu na mji wa Port Sudan. Katika siku mbili zilizopita, mashambulizi mengine ya Droni yaliilenga miji ya Kosti, Rabak na Kenana katika jimbo la Kaskazini mwa Sudan la White Nile pamoja na Al-Damer kaskazini mwa mji mkuu.

Vurugu zauwa watu 38 El-Fashir Sudan

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Shambulio hilo limefanyika baada ya wizara ya mambo ya nje inayoungwa mkono na jeshi kukubali kwa masharti mwaliko wa Marekani kwenye mazungumzo nchini Uswisimwezi Agosti. RSF tayari imejibu ikisema itafanya majadiliano tu na jeshi na sio Waislamu wanaodhibiti kwa kiasi kikubwa sekta ya umma. Juhudi za hapo awali za kusuluhisha mzozo huo zimeambulia patupu na Wasudan wengi wanaona mazungumzo ya Uswisi kama fursa bora ya kumaliza vita.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mzozo huo umesababisha takriban watu milioni 10 katika nchi hiyo iliyoko kwenye Pembe ya Afrika kuyakimbia makazi yao.

 

Related Posts