SIMBA WAUZA TIKETI ZOTE ZA SIMBA DAY 2024 – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Klabu ya Simba imetangaza kuwa tiketi zote zilizoandaliwa kwa ajili ya mashabiki kushuhudia kilele cha Simba Day 2024 kwenye Uwanja wa Mkapa zimeisha.

 

Akizungumzia kufikia tamati kwa uuzaji wa tiketi Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula amesema, ” Simba tumeonyesha ukubwa wetu na tumeweza kuvunja rekodi yetu ya mwaka jana ambapo tuliuza tiketi zote siku mbili kabla ya Simba Day, mwaka huu tumeuza tiketi zote – SOLD OUT siku tatu kabla ya Simba Day.”

 

“Hongereni sana mashabiki wetu na tukutane uwanja wa mkapa kwenye Simba Day ya Ubaya Ubwela. Timu yeyote kubwa inapimwa na ukubwa wa sapoti ya mashabiki wake, na hii inadhihirisha kwanini mashabiki wa Simba mlichaguliwa kuwa mashabiki bora barani Afrika.”

 

Kilele cha Simba Day ni siku ya Jumamosi ya Agosti 3 ambapo Simba watatambulisha wachezaji wao wapya, beachi la ufundi na kisha watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya APR FC ya Rwanda. Mechi itapigwa saa 1:30 usiku ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

Related Posts

en English sw Swahili