Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye pia ni balozi wa mazingira nchini, Peter Msechu amesema kuwa wasanii wengi wamekuwa wakitunga na kuimba nyimbo nyingi zinazohusu mapenzi badala ya kuimba mambo ya msingi yenye maslahi kwa taifa ikiwemo utunzaji wa mazingira, utalii na mengine.
Msechu ameyasema hayo leo Julai 30, 2024 mjini Morogoro akiwa katika shughuli zake za muziki ambapo amesema kuwa yeye ameamua kutumia kipaji chake katika kuisaidia serikali juu ya suala la utunzaji wa mazingira huku akisema kuwa mazingira ndio msingi wa maendeleo kwani bila kuwepo hakuna shughuli yoyote inayoweza kufanikiwa.
“Wasanii wa sasa wengi wanaimba mapenzi, utakuta kwenye albamu nyimbo zote zinahusu mapenzi, wana kazi ya kulalamika tu kwenye nyimbo ‘oooh umeniacha…oooh nakupenda’ mimi siimbi nyimbo za namna hiyo,” amesema Msechu.