Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024
Na Oscar Assenga, TANGA.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Tanga imeanzisha uchunguzi wa miradi minne iliyobainika kuwa na mapungufu ilipozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024.
Akizungumza leo na waandishi wa Habari mkoani Tanga wakati akitoa taarifa utendaji kazi wao kwa kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni 2024 kwa niaba ya Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Afisa Uchunguzi Mwandamizi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Frank Mapunda ambapo alisema kwamba waliendelea na ufuatiliaji utekelezaji wa miradi ya maendeleo 79 yenye thamani ya Milioni 34,517,081,773.60.
Mapunda ambaye pia ni Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Takukuru Mkoa wa Tanga alisema miradi ambayo ilifuatiliwa ni katika sekta za kipaumbele ambazo ni Elimu, Barabara, Maji na Afya pamoja na ile ambayo ilitembelewa na kuzinduliwa au kuwekwa mawe ya msingi katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024.
Aliitaja miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba ya walimu shule ya Msingi Kisinga wenye thamani ya Sh.Milioni 50 katika Halmashauri ya Lushoto, Ujenzi wa Zahanati ya Milingano wenye thamani ya Milioni 553.
Mapunda alitaja mradi mwengine ni upanuzi wa kituo cha Aya Mgwashi wenye thamani ya Milioni 500,000,000.00 na mradi wa zahanati ya Maalie wenye thamani ya Sh.Milioni 50,000,000.00.
Wakati huo huo, Mapunda alisema kwamba katika kipindi hicho walifanya kazi ya uelimishaji kwa wajumbe wa kamati za Afya ya Msingi katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali pamoja na Watumishi na Wataalamu wa Sekta ya Afya ambao ni 485 kwa idadi yao katika wilaya za Kilindi,Handeni,Korogwe na Lushoto.
“Katika uelimishaji huo tuliweka kipaumbele ushirikishwaji wadau katika uzuiaji rushwa kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote katika wilaya hizo ambapo wakuu wa wilaya zote walishiriki kufungua mafunzo na kuhimiza uadilifu,uwajibikaji na huduma bora za Afya ya Msingi katika wilaya zao”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba wataendelea kufanya udhibiti na uzuiaji wa rushwa kwenye eneo la ukusanyaji mapato kwa kushirikiana na mamlaka husika kufanya ufuatiliaji wa moja kwa moja kwenye vyanzo vya mapato vilivyoanishwa katika bajeti kwa kuangalia mienendo ya makusanyo ya mapato sambamba na kushauri hatua mbalimbali za kudhibiti upotevu wa mapato wakati wa mchakato wa ukusanyaji.