Mwisho wa ubishi CAFCL | Mwanaspoti

Pretoria, Afrika Kusini. Mechi za pili za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya nusu fainali zinapigwa leo kwenye viwanja viwili tofauti, hadi saa sita usiku timu zitakazokwenda fainali zitakuwa zimeshafahamika.

Hii ni hatua muhimu kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika, ambapo Al Ahly ambayo iliitupa nje Simba kwenye hatua ya robo fainali, itaingia uwanjani kuvaana na TP Mazembe kwenye mchezo wa pili baada ya ule wa kwanza uliopigwa nchini DR Congo kumalizika kwa suluhu.

Mechi nyingine kali leo itakuwa nchini Afrika Kusini, wakati Mamelodi Sundowns ambayo iliitupa Yanga nje kwenye hatua ya robo fainali itakapokuwa nyumbani kuvaana na ES Tunis kwenye mchezo mwingine, huku mechi ya kwanza iliyopigwa nchini Tunisia ikimalizika kwa Mamelodi kupoteza kwa bao 1-0.

Timu zote hizi zinazomalizia nyumbani, pia zilimaliza nyumbani kwenye michezo ya hatua ya robo fainali, hivyo zina kazi kubwa ya kuhakikisha zinakwenda fainali, ambapo kwa Ahly itakuwa ni mara ya pili mfululizo.

Mashabiki wa soka wanausubiri mchezo huu kwa hamu kubwa baada ya timu zote kuonyesha kiwango cha juu kwenye mechi ya kwanza na hivyo zote zina nafasi ya kwenda fainali.

TP Mazembe ambayo ilipotea kwenye hatua kama hii kwa muda mrefu inakwenda uwanjani ikitafuta ushindi au sare ya mabao ili iweze kuvuka kwenye hatua hii kwenda fainali, huku Ahly ikitakiwa kutafuta ushindi pekee na kama itatokea suluhu basi mikwaju ya penalti itahusika, namba zinasemaje kuhusu timu hizi?

Inatoka uk.20. 2. Al Ahly imefanikiwa kushinda michezo yote miwili ya nyumbani ambayo imevaana na TP Mazembe kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, yote ikiwa hatua ya makundi, mwaka 2002 ilishinda 1-0, na 2012, 2-1.

 5. Al Ahly inatafuta nafasi ya kwenda fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa misimu mitano mfululizo ikiwa ni timu ya kwanza kufanya hivyo. Kama ikifika fainali itakuwa ni mara yao ya 17, huku kukiwa hakuna timu nyingine ambayo imewahi kufika fainali mara kumi kwenye historia ya michuano hiyo.

1. TP Mazembe iliibuka na ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho wa ugenini wa Ligi ya Mabingwa Afrika ilipoichapa Petro de Luanda mabao 2-1, lakini haijawahi kushinda michezo miwili mfululizo ya ya ugenini kwenye michuano hii kwa msimu mmoja.

36.6. Al Ahly ilimiliki mpira kwa asilimia 36.6% tu, kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Mazembe, hiki ni kiwango cha chini zaidi cha umiliki wa mpira kwa timu hiyo kuanzia mwaka 2021, ilipomiliki kwa asilimia 30.2, dhidi ya Mamelodi Sundowns.

7. Ali Maâloul (Al Ahly), amekuwa na asilimia 71 za umiliki wa mpira kwenye mechi zote anazoichezea timu yake.

3. Hussein El Shahat wa Al Ahly anashika nafasi ya pili kwa kupachika mabao kwenye michuano hii msimu huu, akiwa ameshapachika mabao matatu hadi sasa, moja nyuma na Sankara Karamoko mwenye manne.

2. Kiungo Fily Traore wa Mazembe, anashika nafasi ya pili kwa kupiga pasi nyingi zilizozaa mabao msimu huu, akiwa nazo mbili sawa na kinara Anthony Modester wa Al Ahly.

8. Al Ahly imecheza michezo nane kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu bila kuruhusu bao lolote.

 45.TP Mazembe inashika nafasi ya tatu kwa timu iliyopiga kona nyingi kwenye michuano hiyo msimu huu, baada ya kupiga mara 45.

Macho na masikio ya wengi yapo kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld wakati Mamelodi itakapokuwa nyumbani kuvaana na Esperance de Tunis ya Tunisia ambayo inatafuta nafasi ya kwenda fainali baada ya kipindi kirefu.

0-1. Mamelodi Sundowns ilipoteza mchezo wa kwanza wa nusu fainali kwa kulala bao 1-0 dhidi ya ES Tunis, lakini timu hiyo haijawahi kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya mpinzani mmoja kwa msimu mmoja, kwenye hatua ya mtoano.

8. ES Tunis inaweza kufika fainali kwa mara ya nane, ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 2018-19, huku Mamelodi Sundowns ikifika itakuwa ni timu ya kwanza ya Afrika Kusini kufika fainali mara tatu baada ya 2001 & 2016.

 1. Mamelodi Sundowns imepoteza mchezo mmoja tu kati ya 31 iliyocheza nyumbani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, imeshinda 20 na sare 10. ilipoteza dhidi ya  CR Belouizdad, Aprili 2021 (0-2).

4. ES Tunis imegonga mwamba mara nne kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu, ikiwa ni zaidi ya timu nyingine yoyote kwenye michuano hii.

7. ES Tunis haijaruhusu bao kwenye michezo saba iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa imepigiwa mashuti 51 bila kufungwa.

 21. Lucas Riberio Costa wa Mamelodi Sundowns, amekokota mpira mara 21 na  Houssam Ghacha wa ES Tunis, amekokota mara 19, ndiyo wachezaji wanaoongoza kwa kukokota mpira kwenye michuano ya msimu huu.

Related Posts