Kampuni ya Heineken Beverages yapanua soko kwa kuinunua Bia ya Windhoek

Meneja wa Kampuni ya Heineken Beverages International hapa nchini, Obabiyi Fagade (kulia) akiongea katika mkutano na waandishi wa habari,(kushoto) ni , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beers, Wines and Spirits, Jerome Rugemalila

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beers, Wines and Spirits, Jerome Rugemalila (katikati) akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wengine pichani kulia ni Meneja wa Kampuni ya Heineken Beverages International hapa nchini, Obabiyi na kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo Lilian Pascal

KAMPUNI ya kutengeneza vinywaji duniani, Heineken Beverages imetangaza upanuzi wa soko lake la vinywaji vya Heineken nchini Tanzania kwa kuongeza bia ya Windhoek.

Taarifa hiyo rasmi imetolewa katika mkutano na wanahabari uliofanyika leo Julai 31, 2024 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Upanuzi huu wa jalada unafuatia ununuzi wa kampuni ya Namibia Breweries Limited (‘NBL’), mzalishaji wa bia ya Windhoek, na ununuzi wa Distell Group Holdings Limited, kampuni nyingine inayoongoza duniani ya vinywaji, uliofanyika mwaka 2023.

Bia ya Windhoek ni bia ya lager ya hali ya juu inayotengenezwa nchini Namibia ikiwa na ladha nyororo, ya kuburudisha, inayoheshimika kama bia bora zaidi, na iliyo na ubora kamili. Watanzania wanaipenda bia ya Windhoek na sasa tunayo furaha kuiongeza bia hii katika orodha ya bidhaa zetu.

Sambamba na hilo, kampuni ya Heineken Beverages pia imeanzisha ushirikiano wa kimkakati na kampuni ya KiTanzania – Mabibo Beer, Wines and Spirits, ambayo kabla awali ilikuwa na haki ya kipekee ya kuagiza bia ya Windhoek nchini. Mabibo atakuwa msambazaji rasmi wa bia ya Windhoek nchini Tanzania.

Ushirikiano huu wa kimkakati unadhihirisha dhamira ya Heineken ya kusaidia biashara za ndani na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania huku ikisisitiza zaidi dhamira yake ya kuleta thamani ya kiuchumi barani Afrika. Heineken Beverages, ambayo ni muunganiko wa nguvu za Heineken Afrika Kusini, Distell, na Namibia Breweries, inalenga kupata fursa kubwa za ukuaji katika kanda ya Kusini mwa Afrika.

Akizungumzia ununuzi na ushirikiano huo mpya na Mabibo, Meneja wa Kampuni ya Heineken Beverages International hapa nchini, Obabiyi Fagade, alielezea shauku yake akisema, “Ushirikiano huu na Mabibo Beer, Wines and Spirits ni ukurasa mpya wa kusisimua katika safari yetu hapa Tanzania. Kwa kuunganisha utaalamu wetu wa kimataifa kama Heineken na ujuzi mkubwa walionao Mabibo katika soko la ndani, tuna uhakika katika uwezo wetu wa kuwasilisha bidhaa na huduma za kipekee kwa wateja wetu wa Tanzania.”

Heineken Beverages imedhamiria kutoa huduma za kipekee kupitia vinywaji vyenye ubora wa juu ambavyo vinakidhi ladha za watumiaji. Kupitia ushirikiano huu, kampuni inalenga kuimarisha nafasi yake kwenye soko na kuchangia maendeleo endelevu ya tasnia ya vinywaji nchini Tanzania.

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beers, Wines and Spirits, Jerome Rugemalila alisema “Mkataba huu wa kibiashara umekuja baada ya Kampuni ya Mabibo na Namibia Breweries Ltd (NBL) kukubaliana kuvunja mkataba walioingia mwaka 2008.

Kampuni ya Mabibo Beer imefanya kazi na Heineken Beverages na tunafurahi kuwa mmoja wa wasambazaji wa bidhaa za HBI.

Tunaomba washirika wetu wa kibiashara, wadau wetu kuendelea kushirikiana na Mabibo na HBI, hasa ukizingatia kuwa tumeongeza wigo wa bidhaa bora kama Windhoek, Heineken, Desperados, Savanna, Amarula, Drostdyhof n.k. Kwa taarifa hii, HBI inakuwa muagizaji pekee wa bidhaa za Namibia Breweries nchini Tanzania.

Related Posts

en English sw Swahili