Maafisa Usafirishaji wasikilizwa na Polisi Kata Ngara Mjini.

Mkaguzi kata ya Ngara Mjini Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Olipa Chitongo amefika katika kituo cha waendesha Pikipiki ya magurum mawili na kusikiliza kero za kiusalama zinazowakabili huku akiwaomba kuendelea kutoa taarifa Kwa Jeshi la Polisili Juu ya watu wanaofanya uhalifu katani hapo.

Mkaguzi huyo amebainisha hayo mara baada ya kusikiliza kero za kiusalama Kwa madereva hao ambao amewataka kutambua kuwa jamii inawaona kama msaada mkubwa katika sekta ya usafiri ambapo amewaomba kufanya kazi yao kwa misingi ya sheria na kufuata sheria za usalama Barabarani.

Aidha amewataka kutokubali kuchafuliwa na Mtu yoyote ambaye atatumia kivuli cha dereva pikipiki na kufanya uhalifu na badala yake amewataka kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili mhusika achukuliwe hatua.

 

Related Posts